The House of Favourite Newspapers

JPM awaonya wanaoendekeza siasa badala ya kazi

0
magufuli_aapaRais Dkt. John Magufuli
Ikulu, Dar es Salaam;

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, amekabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.

Baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais Magufuli amesema Sh. Bilioni 12 zilizopatikana kama chenji baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kumalizika, zitatumika kujenga jengo jipya la Tume ya Uchaguzi mjini Dodoma.

Rais Magufuli pia amewaonya wanasiasa wanaomchelewesha kufanya kazi ya kuwatumikia Watanzania na kuendekeza siasa.
Amesema haiwezekani uchaguzi umepita na mshindi amepatikana lakini wanasiasa hao wanaendeleza siasa ilhali wananchi wanataka watumikiwe wapate maendeleo. Rais amesema hatawavumilia viongozi wa siasa wenye lengo baya na nchi na kuwataka waweke maslahi ya Taifa mbele badala ya vyama vyao. Amewataka kufanya siasa baada ya miaka mitano ambapo wananchi watawapima kile walichokifanya kwa muda wote huo.
Pia rais Magufuli amesema kuwa marais wastaafu nchini watalindwa dhidi ya tuhuma zote na kuhakikisha hawanyayasiki baada ya kustaafu kwao.
Awali Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema suala la Kura ya Maoni halikusitishwa kama baadhi ya watu wanavyosema bali iliahirishwa kwa kuwa wakati kura hiyo ilipotakiwa kupigwa Aprili Mwaka jana, Tume ilikuwa na jukumu kubwa la kuandaa uchaguzi Mkuu.
Kutokana na hali hiyo, Jaji Lubuva alisema Tume haikuwa na uwezo wa kubeba mambo mawili makubwa kwa wakati mmoja. Jaji Lubuva amesema kutokana na zoezi la Uchaguzi Mkuu kumalizika rasmi, Tume iko tayari kuanza mchakato wa kura ya maoni.
Kuhusu suala hilo la Kura ya Maoni, Rais Dk Magufuli amemhakikishia Jaji Lubuva kuwa serikali italiamualia mara baada ya Tume kulifikisha serikalni.
Leave A Reply