The House of Favourite Newspapers

JPM: CCTV zifungwe mitaani, Waliotumbuliwa na Makonda Wawajibishwe

0

Tanzania's President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania's ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi SaidRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa rai ya kufunga CCTV kwenye mitaa, amesema Kinondoni ndio inasifika kuwa na uhalifu mwingi katika nchi hii. Amesema wilaya ya Kinondoni ilikuwa na vitendo vya uhalifu 8,094 na mwaka 2015 vikafika 8,804 huku akitoa agizo kwa TCRA ambao ndio wana wajibu wa ku-monitor simu zote washirikiane na jeshi la polisi. Asietaka kushirikiana na jeshi la polisi aondoke.

Rais Magufuli ameyasemahayo leo wakati akihutubia kwenye hafla ya Uzinduzi wa Kuboresha Usalama wa Raia, iliyofanyika kwenye Viwanja vya BIAFRA, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo Rais Magufuli alikuwa Mgeni Rasmi.

Mbali na hayo, rais Magufuli ameviagiza vyombo vya usalama nchini kuwachukulia hatua za kisheria mara moja makandarasi wote na injia ambao jana waliosimamishwa kazi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kujenga barabara chini ya kiwango jijini Dar es Salaam.

Magufuli (1) Rais Magufuli na Wageni Waalikwa, wakiwa Meza Kuu

Jana, June 24, 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alizisimamisha kazi na kusitisha mikataba ya Kampuni ya Inshinomya Co. LTD na kuyasimamisha Makampuni mengine ya kujenga barabara ya Germinex construction LTD, Del Monte (T) Ltd na Skol Building Contraction.

Kutokana na kujenga barabara chini ya kiwango na kuagiza makampuni hayo kutopewa tenda yeyote kwenye Mkoa wa Dar es Salaam mpaka Mkuu wa Mkoa atakapojiridhisha na utendaji wa kazi kwa makampuni hayo.

Mwigulu (6)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, akisalimiana na wageni na viongozi walifika kwenye hafla hiyo.

Miongoni mwa waliofika kwenye hafla ya Uzinduzi wa Kuboresha Usalama wa Raia Viwanja vya BIAFRA ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Magufuli, Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mridho Kikwete, Katibu Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi John W.H. Kijazi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu, mwenyekiti wa mkoa Dar es Salaam, Madabida na wengine wengi.

Magufuli (2)Sehemu ya Umati wa wananchi waliohudhuria

Mzungumzaji aliyepita ni mkurugenzi wa CRDB, Dr. Charles Kimei na miongoni mwa mambo aliyogusia ni utumbuaji majipu.

IGP Mangu: Mangu amemshukuru Rais Kikwete kwani mpango wa kuliboresha jeshi la polisi ulibuniwa wakati wake.

Tutakaa na wataalam ili kubuni vyanzo fedha ili kutimiza tuliyoyapanga na ni mkakati ili kuboresha huduma tunazozitoa kwa wananchi na kero zote kwa jamii. Mangu anasema wakati Magufuli anafungua bunge alisema ‘Serikali nitakayoiunda nataka ihudumie jamii kwa haraka’ hivyo mpango wao unajibu hilo tatizo.

Amesema mkuu wa mkoa asaidie pia wananchi watakuwa wamejisaidia wenyewe kwa kuweka taa kwenye nyumba zao mbele na nyuma kwani jiji la Dar es Salaam liko kwenye giza. Mangu anasema Bilioni 27 zinahitajika ili jiji la Dar es Salaam liwe kwenye kiwango cha juu cha usalama pengine kuliko majiji yote Afrika.

Mwigulu (4)Kutoka kulia ni Rais John Magufuli, Waziri Mwigulu Nchemba na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete.

Mwigulu Nchemba: Mwigulu amewataka wananchi wawe wanatoa taarifa ili kuzuia uhalifu, amemuomba Rais Magufuli kupata fedha za kuweza kutekeleza mpango wa jeshi la polisi ili kuundoa uhalifu kwenye jiji la Dar es Salaam ambayo pia itavutia wawekezaji. Amesema hadhara sio ya kwake na alikuwa anachomeka, anamkaribisha Rais Magufuli.

“Hamna demokrasia ambayo haina mipaka, mpango wa jeshi la polisi unatarajia kuanza utekelezaji wake Julai 1, 2016.” Alisema Mwigulu.

Rais Magufuli: Kwa niaba ya watanzania, niwashukuru wananchi wa Dar kwa kuweza kuacha shughuli zenu na kuja kuhudhuria, wateni wenzangu wakwere wanasema shughuli ni watu. Nawashukuru CRDB, NMB pamoja na Super doll ambao wakurugenzi wao wako hapa, pia nashukuru nchi ya Malaysia ambao ndio wamesaidia uanzishwaji wa big results now(BRN) na mimi nakushukuru kwa kuona matokeo ya big results now.

Nashukuru watu wa Biafra kwa kunipa kura nyingi ambapo nilifanya kampeni na kufanikiwa kuwa Rais mpaka natamani kuanza kampeni lakini uchaguzi umekwisha.

Rais Magufuli alishangazwa kutomuona Meya wa Kinondoni, Boniphace Jacob kwenye uzinduzi wa Mpango wa Usalama wa Jamii Viwanja vya Biafra Dar. Baada ya kumuita Mstahiki Meya wa Kinondoni aje asalimie kwani ujambazi hauna chama (Hayupo). Badala yake akamuita Diwani wa Kinondoni (CHADEMA) ambaye aliamka na kwenda kuwasalimia wananchi.

Rais Magufuli amehoji kwanini jambazi aende kufanya ujambazi bila kupokonywa bunduki yake haraka wakati wao pia wana bunduki. Ametoa wito kwa polisi wote nchini, jambazi akienda sehemu na bunduki kufanya uhalifu, apokonywe bunduki yake haraka na polisi wanaowapokonya majambazi bunduki haraka wasipelekwe mahakamani, wapandishwe cheo kwani wananchi wamechoka.

Amesema jeshi la polisi wakiamua Tanzania kuwe na amani, kutakua na amani. Amesema vijana wanaweza kuwa na hamu ya kufanya kazi lakini maofisa wa polisi wanawabana bana. Rais amezungumzia mchezo wa kuvujisha taarifa za wanaotoa taarifa za uhalifu na kukemea.

Rais amesema pia waliotoa msaada, wakitokana na ujambazi pia wakamatwe. Amesema yeye hatumbui majipu lakini yanajitumbua yenyewe na kutoa wito kwa watanzania wote kuendelea kuliamini jeshi la polisi, kushirikiana nalo na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.

Rais Magufuli ametoa pongezi kwa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete na IGP mstaafu kwa kubuni mpango huo na kuzaa matunda. Amesema amedhamiria kuijenga nchi kwa nguvu zake zote na atafanya kazi kwa nguvu zake zote na hatabagua mtu.

Rais ametaka Tupeleke maendeleo mbele na kuweka vyama pembeni na kulishukuru bunge kwa kupitisha muswada wa mafisadi ili wanyooke. Amesema alikuwa anachomekea na atarudi siku rasmi kuzungumzia hilo swala.

Leave A Reply