The House of Favourite Newspapers

JUICE KINGDOM YAZIDI KUKUBALIKA MITAANI!

SIKU chache baada ya kuzinduliwa vinywaji vya Juice Kingdom tawi la Tabata-Segerea, taarifa ni kwamba vinywaji hivyo vinazidi kukubalika kwenye mitaa mbalimbali.

Tawi hilo la Juice Kingdom lilizinduliwa Septemba 14, mwaka huu ambapo watu mbalimbali za juisi hizo ambazo zinatengenezwa na matunda halisi bila kuongeza kemikali ya aina yoyote.

Wakazi mbalimbali wa Segerea waliozungumza na Ijumaa mara baada ya kuonja juisi za Kingodom, walisema ina ladha ya kipekee na hawajawahi kuipata mahali popote nchini.

Mmoja wa wakazi ambao walifika eneo hilo, Aisha Kiokote, alisema wanawashukuru Juice Kingdom kwa kuwasogezea huduma hiyo kwani wameikosa kwa miaka mingi.

 

“Hapa ilikuwa ukitaka juisi lazima uende mbali sana lakini sasa tumeipata juisi nzuri tena yenye viwango vya hali ya juu,” alisema Aisha.

Mkurugenzi wa Juice Kingdom, Zabron Julius amesema wameamua kuanzisha tawi hilo ili kuwasogezea huduma wakazi wa maeneo hayo kwani walikuwa wakilazimika kwenda mbali kufuata juisi zao.

 

“Tuna matawi sehemu mbalimbali kama Sinza na Mikocheni sasa kwa Tabata tulikuwa hatujafika, sasa wakazi wa Tabata Segerea na maeneo jirani watafurahia juisi zetu,” alisema Zabron.

 

Alisema, tofauti na matawi yake mengine yaliyopo katika kona mbalimbali za jijini Dar, tawi hilo la Tabata- Segerea lina nyama choma, baga, kuku na vyakula mbalimbali pamoja na bia!

 

“Yani mteja atachagua yeye tu kama amekuja na wenzake ambao pengine wanatumia bia, yeye anatumia juisi basi chaguo ni lake,” alisema Zabron.

 

 

Alisema ukifika kwenye vituo vyao, utapokelewa na wahudumu nadhifu, wachangamfu kiasi cha kukufanya ujisikie upo nyumbani.

 

Alisema juisi hizo zinapatikana kwa ukubwa na bei tofauti hivyo mteja kujinunulia kulingana na saizi anayoitaka.

 

STORI: MWANDISHI WETU

 

LIVE PERFOMANCE: Young D Kwenye Uzinduzi wa Kingdom Juice

Comments are closed.