The House of Favourite Newspapers

Justin Bieber amrudia Mungu

0

beiberJustin Bieber

BOSTON, Marekani
KWA sasa mwanamuziki, Justin Bieber yupo kwenye zoezi maalum la kuhakikisha anarejesha utu wake na kupata baraka za Mungu na kuamua kujitenga akifanya mambo yanayotafsiriwa kuwa labda ana matatizo ya akili.
justin
Kwa mujibu wa watu wa karibu na staa huyo, ni muda wa wiki mbili sasa Bieber amekuwa haonekani kwenye matamasha ya muziki wala katika kumbi za starehe zaidi ya kutumia muda wake mwingi akiwa kwenye majani, miti na kutembelea sehemu wanakopatikana wanyama wasio wakali.

Bieber amewaeleza rafiki zake kuwa amepoteza mwelekeo na kuna kitu anahisi anakikosa hivyo kukaa karibu na uoto wa asili na wanyama huku akijaribu kuzungumza na Mungu wake kunaweza kumrejesha kwenye hali nzuri.

Pamoja na hayo, kumekuwa na video na picha mbalimbali za hivi karibuni zikimuonyesha Bieber akifurahia kupanda juu ya miti na kutembea kwenye bustani.

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply