The House of Favourite Newspapers

Justine Bieber Athibitisha Kupooza Uso, Aahirisha Shoo Zake

0
Muonekano wa Justine Bieber baada ya kupooza upande mmoja wa uso

MWANAMUZIKI raia wa Canada, Justin Bieber (28) amefichua kuwa anaugua ugonjwa wa kupooza usoni baada ya matamasha yake kuahirishwa wiki hii.

Justin amethibitisha hayo kwenye video fupi katika ukurasa wake wa Instagram ambao una wafuasi milioni 240, kwamba hali hiyo ni kutokana na kugunduliwa kuwa ana ugonjwa unaoitwa Ramsay Hunt.

Bieber akiwa na mpenzi wake

“Kama unavyoona jicho langu halikonyezi, siwezi kutabasamu upande huu wa uso wangu… Kwa hiyo kuna kupooza kabisa upande huu wa uso wangu,” amesema.

 

Mapema Wiki Hii Tamasha la Muziki la Justice World Tour lililoandaliwa na Justine Bieber ambalo lilianza mwezi Februari imetangazwa kuwa Shoo tatu zimeahirishwa.

 

Ni kutokana na virusi hivi ambavyo vimeshambulia neva za sikio na uso wangu ambavyo vimesababisha kupooza kwa sehemu yangu ya uso hili ni jambo nyeti sana kwahiyo nawaomba mashabiki msubiri kwasasa sipo sawa. Alisema Bieber

 

 

Leave A Reply