The House of Favourite Newspapers

JUSTINE BIERBER AFUNGULIWA MASHTAKA YA KUMNYANYASA MNENGUAJI WAKE

Image result for justin bieber

MWANAMUZKI wa miondoko ya Pop Justine Bierber yupo kwenye tuhuma nzito za kumnyanyasa mnenguaji wake wa kike Emma Portner , kupitia insta story ya mnenguaji uyo aliweka ujumbe wenye tuhuma nzito za Justine Bierber pamoja na kutomlipa mshahara wake.

Image result for Emma Portner

Emma Portner ameshiriki kucheza kwenye Video zote za album ya ‘Purpose’ pamoja na ziara yake ‘Purpose Tour’ lakini ilifika kipindi alikosa hadi pesa ya kula kutokana na Justine Bierber kutomlipa pesa yake inavyostshili.

Justine Bierber anaibagua jamaii inayoshiriki mapenzi ya jinsia moja  huenda hii ikawa sababu ya Justine Bierber kutomlipa Emma Portner ambaye anashiriki mapenzi ya jinsia moja (Lesbian) .

“Huwa unaenda kwenye makanisa ambayo hayaungi mkono jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ) lakini kwenye kampuni yako umeajiri ‘Lesbian’ tena anafanya video pamoja na show zako, Unajisikiaje? Halafu unamlipa kiasi kidogo tu cha pesa?” aliandika Emma Portner.

Alimaliza ujumbe wake huo mzito kwa kumtaja na Chris Brown kwamba wanapaswa kuwajibishwa kwa uonevu dhidi ya wanawake.

Comments are closed.