The House of Favourite Newspapers

NIYONZIMA KUIBUKIA CONGO

IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba, Haruna Niyonzima yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu ya AS Vita ya Congo na APR ya Rwanda.

 

Niyonzima amewaaga mashabiki wa Simba na kusema kuwa, hivi karibuni atataja timu atakayoenda huku tetesi zikieleza kwamba ana nafasi kubwa ya kutua Congo.

 

Imeelezwa kuwa timu hiyo iliutambua uwezo wa Niyonzima baada ya kucheza na timu ya Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Comments are closed.