The House of Favourite Newspapers

JUX Apokelewa kwa Shangwe Global Group (Picha + Video)

MSANII  wa Bongo Fleva, Juma Mussa maarufu kama (Juma Jux), leo Novemba 19, 2019 amepokelewa kwa shangwe na wafanyakazi wa Global Group alipofika kufanya mahojiano na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia kutoka +255 Global Radio kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni.

 

Meneja Vipindi wa +255 Global Radio, Borry Mbaraka (kulia) akisalimiana na  Msanii wa Bongo Fleva, Juma Mussa maarufu kama (Juma Jux) wakati alipotinga Ofisi za Global Group.
Meneja Vipindi wa +255 Global Radio, Borry Mbaraka (kushoto) akimpa maelekezo Jux pamoja na timu yake alioykuwa ameongozana naoyo baada ya kusaini kitabu cha wageni.
Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Richard Manyota (kushoto) akizungumza jambo na Msanii Jux wakati alipotembelea ofisi hizo.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Sifael Paul (kushoto) akisalimiana na Msanii Jux wakati alipotembelea ofisi hizo za Global Group.
Mhariri wa Gazeti la Championi, Ezekiel Kitula (kushoto) akisalimiana na Jux wakati alipotemebelea Idara ya magazeti ya michezo yanayochapishwa na kampuni hiyo.
Mwandishi wa habari za michezo, Sharifa Mmasi( kulia) akipozi na Msanii Jux wakiwa wameshikilia Gazeti la Championi.

 

Mwandishi wa habari za Michezo, Mussa Mateja (kulia) akipozi na msanii Jux akiwa ameshikilia Gazeti la Michezo mahususi kwa masuala ya kutoa mwongozo katika masuala ya kubeti.
Mkuu wa Kitengo Cha Global Tv Online, Abdallah Ng’anzi (kulia) akimpa taarifa fupi Msanii Jux juu ya kitengo chake kinavyofanya kazi kupitia waandishi wake mahiri kuhakikisha wananchi wanapata habari kwa wakati.
Msanifu kurasa za magazeti, Charles Mgela (kulia) akisalimiana na Jux.

 

Msanii huyo akiwa kwenye ofisi hizo amejionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ikiwemo suala la uandaji wa magazeti na masuala mengine ya kuhakikisha kampuni hiyo inahabarisha umma kupitia vyombo vyake ikiwemo mitandao ya kijamii.

 

Akiwa kwenye studi za +255 Global Radio aliweza kuzungumzia albam yake ‘The Love Album’ namna inavyofanya vizuri katika soko na kuwataka mashabiki zake kuendelea kumuunga mkono.

 

 

Comments are closed.