The House of Favourite Newspapers

JUX: VEE MONEY KWANGU NI KILA KITU

Juma Khalid ‘Jux’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’

MKALI wa Muziki wa R&B Bongo, Juma Khalid ‘Jux’ amesema msanii mwenzake ambaye pia ni mpenzi wake, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ kwake ni kila kitu kutokana na kumsapoti katika muziki wake.

Jux aliiambia Risasi Vibes juzikati wakati akisherehekea bethidei yake iliyofanyika ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar kuwa, muziki kwake ni kazi na pia upo kwenye damu hivyo anamshukuru Vee Money pamoja na wazazi wake kwa sapoti yao kubwa wanayoionesha kwake.

“Kiukweli namshukuru Mungu kwa sababu nimejikuta nimezaliwa na kipaji cha uimbaji na pia wazazi wangu wamekuwa wakinipa sapoti kubwa kwenye kazi yangu na pia mpenzi wangu Vee Money, amekuwa mtu muhimu sana na kila kitu katika maisha yangu,”alisema Jux.

NEEMA ADRIAN

Comments are closed.