The House of Favourite Newspapers

K-Vant ndani ya chupa mpya yazinduliwa mkoani Arusha

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega, (kulia) akiwa na Meneja mauzo wa Masoko wa Mega Beverages Company Limited, Marco Maduhu wakiingia ukumbini wakati wa hafla ya uzinduzi wa K-Vant ndani ya chupa mpya mkoani Arusha.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega (kulia), Marco Maduhu (Katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Mega Beverages Company Limited, James Kimaro.
Wafanyakazi wakigonga Glasi ya kinywaji cha K.Vant na mgeni rasmi kufurahia mafanikio ya kampuni yao.
Afisa Tawala wa Mkoa Arusha katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Mega Beverages Company Limited na baadhi ya wadau wa kampuni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mega Beverages na wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja.

KAMPUNI ya Mega Beverages Company Limited, yenye makao yake makuu mjini Arusha, imezindua chupa mpya za kinywaji chake cha K-Vant mkoani Arusha, katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru.

 

Uzinduzi wa Arusha unafuatia uzinduzi mkubwa uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema wiki iliyopita.

Meneja Mauzo na Masoko wa kampuni hiyo, Bw. Marco Maduhu alisema “Tunayo furaha kubwa kuwashirikisha wateja wetu katika uzinduzi huu wa chupa yetu mpya hapa mkoani Arusha ambapo tunapaita nyumbani kwetu. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa washirika wetu katika biashara, wadau na wateja wetu kwa kuendelea kutuunga mkono”, alisema.

 

 

Mbali na uzinduzi uliofanyika Dar es Salaam na Arusha, alisema uzinduzi mwingine wa chupa mpya utafanyika mkoani Mwanza, ingawa usambazaji wa bidhaa za K-Vant ndani ya chupa mpya tayari umeanza kufanyika nchini kote.

 

 

Maduhu alieleza pia kuwa Mega Beverages Company Limited, itaanza kufanya kampeni kubwa ya kuendeleza masoko ya bidhaa zake, ambayo italenga masoko ya ndani na masoko katika nchi za Afrika Mashariki, kuhakikisha zinapatikana kwa urahisi mahali pote.

 

 

Kampeni hiyo inatarajiwa kufanikisha ongezeko la uzalishaji, hali ambayo itawezesha kampuni kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuchangia kukuza uchumi wa nchi.

 

Comments are closed.