The House of Favourite Newspapers

Kabila la Wala Watu-14, Vyombo vya dola viliamini kwamba Wazungu hao waliliwa na binadamu wenzao

Na ELVAN STAMBULI| GAZETI LA UWAZI| MAKALA

BAADA ya kuelezea miji na idadi ya watu katika Kisiwa cha Papua New Guinea kilichokithiri kwa baadhi ya makabila nchini humo kula binadamu wenzao, leo tutaangalia jinsi Mjerumani mmoja na msichana wake Mfaransa walivyoliwa mwaka 2008.

Ni Stefan Ramin (40), (pichani) mzaliwa wa Humburg, Ujerumani aliyekuwa na rafiki yake wa kike (girlfriend) Mfaransa aliyetambulika kwa jina la Heike Dorsch (37). Hawa walipotea katika visiwa hivyo baada ya kuingia kwenye msitu walipokuwa wakimtafuta mbuzi wao. Ajabu ni kwamba, walipokuwa wakimtafuta mnyama huyo walikuwa na mwongozaji wa watalii, Henry Haiti  ambaye kitaalamu huitwa  guide.

Walitoweka kwa kustaajabisha kabisa lakini mabaki ya miili yao ilionekana baada ya wiki moja ikiwa pamoja na nguo walizokuwa wamezivaa. Inaamini kwamba Henry ndiye mtu wa mwisho kuwaona Wazungu hao wakiwa hai katika milima ya Nuku Hiva ambako walikwenda kusaka mbuzi.

Walipanga kuishi katika eneo hilo kwa siku kadhaa. Swali lilikuwa ni nani aliyewaua Wazungu hao na kuwanyofoa viungo vyao? Je, ni makabila yale yanayokula watu? Vyombo vya dola viliamini kwamba Wazungu hao waliliwa na binadamu wenzao.

“Uwezekano ni kwamba watu hawa waliuawa na makabila yanayokula watu (Wakorowai na Wafure) na wamekula nyama zao,” alisema kiongozi mmoja wa polisi.

“Inawezekana waliwabanika kwani kuna sehemu ilionesha kuna majivu na kuna mabaki ya meno na mifupa ya mtu na vyote vimechukuliwa na polisi kwa ajili ya vipimo vya DNA,” liliandika Gazeti la Dail Mail likimkariri  Naibu Meya wa Jimbo la Nuku Hiva lenye wakazi zaidi ya 2,000, Deborah Kimitete.

“Hakuna anayeamini kutokea kwa tukio hili baya. Halijawahi kutokea tukio kama hili la kutisha katika eneo hili,” aliongeza.

Aliongeza kwamba yule muongoza watalii Henry, naye anatafutwa na polisi na askari jeshi wa nchi hiyo kwani inadhaniwa kuwa alikula njama na wenyeji wala watu hao ili Wazungu hao waliwe kwa mujibu wa mama mmoja wa kizungu aliyeshuhudia tukio hilo lakini akafanikiwa kutoroka na kutoa taarifa polisi.

“Yule msichana wa kizungu alijaribu kuwasha alam, lakini yule mwenyeji wao Henry alimzuia,” alisema mama aliyetoroka kuuawa. Tayari polisi imetoa askari 22 kwa ajili ya kuwasaka wauaji hao na kuwatia mbaroni na Mzungu huyo wa kike aliwaambia polisi kwamba muongozaji huyo alishiriki kwa karibu sana kuwakamata Wazungu hao na alitumika kumfunga kamba kwenye mti mwanamke yule wa kizungu (Heike).

Kwa mujibu wa habari hizo, majivu na mabaki ya miili ya watu hao ilichukuliwa na mamlaka husika na yakapelekwa Paris nchini Ufaransa kwa ndege kwa uchunguzi zaidi wa DNA. Kati ya Wazungu hao wawili, yule wa kike, Mfaransa alikuwa na habari ya kuwepo kwa makabila yanayokula watu tangu siku nyingi kama alivyoeleza msafiri na mwandishi mmoja aliyekuwa huko aitwaye John Gimlette.

“Waliuawa kikatili sana. Kwanza, waliwavunja miguu yao ili kuwazuia au kuwafanya wasiweze kukimbia kisha wakawavunja mikono
ili kuwavunja nguvu ya kujihami. Huu ni uuaji wa kikatili sana unaofanywa na watu wa Kisiwa cha Marquesans ambacho ni moja ya visiwa vya Papua New Guinea ambao kwao hufurahi kuona mateka wao wakiuawa.

“Hata hivyo, mwisho wa yote waliwaua na kuwachemsha na miili mingine wakairosti,” alisema msemaji mmoja wa polisi.

Serikali ya Ujerumani ilithibitisha kupata habari hizo za kusikitisha na ikasema inafanya mawasiliano na serikali ya visiwa vya Papua New Guinea. Kupotea kwa Wazungu hao kunafananishwa na Mwamerika mmoja alivyopotea kiajabu baada ya kutekwa lakini mabaki yake yakakutwa juu ya wali  kwa wenyeji wala watu wa makabila ya huko.

Wachunguzi wa mambo ya kale wanasema kwamba tukio kama hilo liliwahi kutokea Amerika ya Kusini katika karne ya 20.

 

Comments are closed.