The House of Favourite Newspapers

Kagame Kuanza Leo, Waamuzi 18 Kuchezesha

 

Kikosi cha timu ya Azam SC.

BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limetangaza kuwa, katika michuano ya Kagame inayotarajiwa kuanza leo Ijumaa, itachezeshwa na waamuzi 18 kutoka mataifa mbalimbali.

 

Michuano hiyo ambayo imepangwa kufanyika kwenye viwanja vya Taifa na Azam Complex jijini Dar es Salaam, itahitimishwa Julai 13, mwaka huu.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema mbali na kuwatangaza waamuzi hao, lakini haitavumilia kuona timu shiriki zikileta wachezaji vijana chini ya miaka 20.

 

“Waamuzi tayari tumewaandaa ambapo watakuwa 18 kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mashindano. Kikubwa tunataka kuwa na mashindano yenye ushindani.

 

“Nizikumbushe timu shiriki tu kuwa, zinapaswa kuja na vikosi vyao kamili na hatutavumilia endapo ikitokea timu imeleta kikosi cha vijana chini ya miaka 20,” alisema Musonye.

Comments are closed.