Kagera Sugar: Tunamtaka Aishi Manula

Kocha wa Aishi Manula.

KIKOSI cha Simba hivi sasa kipo katika maandalizi kabambe ya kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Septemba 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

 

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime ameliambia gazeti hili kuwa kesho Jumamosi watapambana na Mbao FC na baada ya hapo wataanza maandalizi ya kujiandaa na mechi ya Simba lakini katika mchezo huo watafurahia zaidi kama Simba itampanga golini kipa wake namba moja, Aishi Manula.

 

Alisema endapo Simba itampanga Manula katika mchezo huo anaamini wataibuka na ushindi kwa mara nyingine kwa sababu anaujua vilivyo udhaifu wake anapokuwa golini na ndiyo maana wamekuwa wakipata matokeo mazuri
kila wanapokutana naye uwanjani.

“Tunaendelea na maandalizi yetu kwa ajili ya mechi yetu na Simba, tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi kwa njia yoyote ile katika mchezo huo.

 

“Kama Simba watamuanzisha Manula golini basi mchezo utakuwa rahisi kwetu kwa sababu ninajua udhaifu wake na nimeshawafundisha wachezaji wangu jinsi ya kukabiliana naye,” alisema.


Loading...

Toa comment