The House of Favourite Newspapers

Kagera Wamkumbuka David Burhani

NA MWANDISHI WETU | CHAMPIONI

WIKI chache baada ya kufariki kwa kipa wa Kagera Sugar, David Burhan, timu hiyo juzi ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Eleven Stars ambao ulikuwa maalum kwa kumuenzi nyota huyo.

Katika mchezo huo, Kagera Sugar ilishinda mabao 3-0, mechi ilipigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kocha Msaidizi wa Kagera, Ally Jangalu amesema kutokana na umuhimu aliokuwa nao mchezaji huyo katika timu hiyo ndiyo maana wameamua kumuenzi kwa kucheza mchezo huo wa kirafiki.

“Sisi kama Kagera Sugar tumeamua kucheza mchezo huu wa kirafiki kwa lengo la kupitia harambee ya kuichangia familia ya marehemu lakini pia kumkumbuka kupitia mchezo huu wa kirafiki,” alisema Jangalu.

Naye Kocha Mkuu wa Eleven, Bantu Moses, amesema wamefurahi kucheza mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa kumkumbuka Burhan ambaye alifariki akiwa anapatiwa matibabu.

Ikumbukwe kuwa, Burhan alifariki Januari 30, mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza  ambapo alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kusumbuliwa na maini kushindwa kufanya kazi pamoja na mapafu kujaa maji.

Save

Comments are closed.