The House of Favourite Newspapers

Kagera Yafikisha Asilimia 97 Sensa, Chalamila Atema Cheche

0
RC Albert Chalamila

WAKATI leo ikiwa ndiyo siku ya mwisho ya sensa nchini mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila, amesema kuwa mkoani kwake wamefikia asilimia 97.4 hadi sasa.

 

Mkuu wa Mkoa huo amesema kuwa makadirio yaliyofanywa na mtakwimu mkuu wa serikali ilikuwa ni kaya 644,655 za mkoa huo ambapo mpaka leo tarehe 29, August saa mbili asubuhi tayari kaya 631,858 zimehesabiwa na nyingine zilizobaki zinaendelea kuhesabiwa.

RC Chalamila akiwa na Karani wa sensa

Amesema changamoto zinazoukabili mkoa huo katika zoezi la sensa ni ukesefu wa umeme katika baadhi ya vijiji, hivyo kusababisha kucheleweshwa kufika kwa taarifa kutokana kuzima kwa vishikwambi lakini walifanikiwa kukodi jenereta na kununua power bank ili kuraisisha utendaji wa kazi.

 

Pia amesema kuwa changamoto nyingine ni Wilaya ya Muleba kuwa na visiwa vingi  pia miundombinu isiyoridhisha lakini wamejitahidi kutatua tatizo hilo,  mkuu wa mkoa  huo amesisitiza kuwa hakuna mwananchi katika mkoa wake atakayebaki na waliobaki wataesabiwa leo.

 

Imeandikwa na:Oswald Mwesiga kwa msaada wa kimitandao.

Leave A Reply