The House of Favourite Newspapers

Kagere Afichua siri ya kuwatungua Yanga

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere, amesema kuwa amewafunga Yanga kwa kuwa anatumia akili katika kufunga mabao na siyo uzee wake kama baadhi ya mashabiki wanavyodai.

 

Kagere juzi Jumamosi aliibuka shujaa wa Simba katika mchezo wa watani wa jadi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Simba Iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Kutokana na ushindi huo, Simba imefikisha pointi 38 na kupanda hadi kwenye nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Yanga wanaongoza wakiwa na pointi 58 wakifuatiwa Azam wenye pointi 49 katika nafasi ya pili. Lakini Simba ina viporo nane kabla ya kufikia idadi ya mechi za Yanga. Na kama wakishinda viporo vyote, wataongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano.

 

Akizungumza Championi Jumatatu, Kagere alisema kuwa anaamini kufunga kwake kunatokana na akili anayoitumia uwanjani, huku akisisitiza kuwa wanataka kushinda kila mchezo.

 

“Kwanza huwa najipa changamoto mwenyewe lakini pia nimebarikiwa na Mungu, kuhusu wanachokisema wao kuwa mimi ni mzee siwezi kujali, kwa kuwa naifanya kazi yangu vizuri.

 

“Wanatakiwa wajue kwamba, umri siyo unaocheza, zaidi ni akili ndiyo inatumika na ndiyo sababu nimefunga, hili tumeshamaliza na limekuwa historia kwa sababu malengo yetu ni kupata pointi tatu katika kila mchezo,” alisema Kagere.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Comments are closed.