The House of Favourite Newspapers

Kagere Aweka Rekodi, Apiga Mabao 69

0

REKODI ya mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, katika upachikaji wa mabao inatisha kutokana na straika huyo kufunga mabao 69 katika misimu minne, jambo ambalo ni ngumu kufanywa na mshambuliaji wa kawaida.

 

Kagere ameweka rekodi hiyo katika klabu mbili tofauti kutoka nchi mbili tofauti yaani Kenya akiiwakilisha Gor Mahia na Tanzania katika klabu ya Simba.

 

Kagere katika klabu ya Gor Mahia ambayo alidumu kwa misimu miwili alifanikiwa kufunga mabao 27, huku akiwa na Simba akifunga mabao 42 katika misimu miwili huku mmoja ukiwa bado haujakamilika.

 

Kagere katika ligi ya Kenya alifanikiwa kuwa mchezaji bora katika msimu wa mwaka 2016-17 baada ya kufanikiwa kufunga mabao 14 huku timu yake ya Gor Mahia ikichukua ubingwa wa ligi kuu.

 

Kwa upande wa ligi ya Tanzania Kagere alifanikiwa kuibuka mfungaji bora katika msimu uliopita kwa kufunga mabao 23 huku msimu huu akiwa kafunga mabao 19 katika michezo 28 ambayo Simba wamecheza hadi sasa.

 

Rekodi hiyo ya mabao inaweza ikaongezeka endapo ligi itataendelea kwani Simba imebakisha michezo 10 ili kumaliza michezo yao yote ya msimu huu.

 

Pia kama ataendelea kubaki katika kiwango alichaonacho kwa misimu mingine zaidI huenda tukashuhudia akiweka rekodi kubwa zaidi.

Stori na Issa Liponda na Marco Mzumbe

Leave A Reply