The House of Favourite Newspapers

Kaizer Chiefs Yamtangaza Kocha Molefi Ntseki, Nabi Apigwa Chini

0
Molefi Ntseki

Klabu ya soka ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini hapo jana imemtangaza rasmi Molefi Ntseki kuwa ndiye kocha wao mkuu atayekinoa kikosi cha klabu hiyo msimu ujao.

Kutokana na hatua hiyo, ni wazi kwamba klabu hiyo ya Kaizer Chiefs imeamua kuachanana na mpango wake wa kumsajili Nassredine Nabi ambaye alikuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga kwa msimu uliopita ambapo Nabi akiwa na wananchi Yanga, alifanikiwa kuwafikisha mpaka hatua ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Nassredine Nabi

Kutokana na maamuzi ya Kaizer Chiefs, Kumekuwa na tetesi mbalimbali ambazo zinaeleza kwamba Kaizer Chiefs wameamua kuachana na kocha huyo ambaye ni raia wa Tunisia baada ya kushindwa kuafikiana hususani katika suala linalohusiana na benchi la ufundi.

Katika suala hilo, kocha Nabi aliomba kwenda na watu wake watatu huku Kaizer Chiefs wakisisitiza kwamba aende na mtu mmoja na kisha wengine atawakuta kule kule.

WHOZU AKATAA KUOA MBELE ya WEMA SEPETU – ”SIJAFIKIA STAGE ya KUOA, JINA LA WEMA ni GENI KWANGU”…

Leave A Reply