The House of Favourite Newspapers

KALANGA Awajibu CCM Walioandamana Monduli – Video

Kufuatia maandamano yaliyofanywa jana na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Monduli mkoani Arusha wakimtaka Mwenyekiti wa chama hicho wilayani humo kueleza sababu za kumpa nafasi, Julius Kalanga ya kugombea tena Ubunge katika jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM.

 

Awali Mh Kalanga alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo hilo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kabla ya kujivua uanachama na kuhamia CCM Ambapo amepoteza sifa ya kuendelea kuwa Mbunge tena na hivyo imelazimika uchaguzi wa marudio kufanyika jimboni hapo.

 

Global TV imemtafuta mwanasiasa huyo na kuzungumza nae kuhusiana na uamuzi wake wa kurudi CCM na maandamano hayo yaliyofanywa na Wanachama wenziye ya kumkataa asiwe muwakilishi tena wa Ubunge katika jimbo hilo kwa Tiketi ya CCM.

VIDEO: MSIKIE KALANGA AKIFUNGUKA

Comments are closed.