The House of Favourite Newspapers

kama hujafikishwa, paza sauti usikike!

0

LOVE2HABARI za leo wapendwa wasomaji wa safu hii, maana tunapozungumza, tayari tupo katika mwezi wa pili ndani ya mwaka mpya. Ni kama juzi tu tulipopigapiga makopo kuukaribisha mwaka mpya.
Shangingi mstaafu nipo na mashosti zangu ambao hupenda kuwadanganya waume au marafiki zao wa kiume kuwa wameridhishwa vilivyo wakati wa mlo wa usiku, wakati ukweli ni kuwa hamna lolote walilojisikia!

Hili jambo lipo sana, tena sana na wala msikatae. Shosti kwa sababu zako, pengine kutaka kumfurahisha mwenzi wako, au aibu, au uoga usio na maana, unamwambia mwenzio kuwa mechi ilikuwa barabara, yaani umefurahi hadi basi, wakati ukweli amekigusa tu kipele, wala hajakikuna!

“Jamani Baby, yaani umenipandisha Mlima Uluguru hadi nimefika, nimefurahije!” utakuta shostito anamwambia mumewe baada ya gemu.

Na unaweza kukuta siku hiyo shosti hata hayo mawazo hayapo hapo, ila tu anaamua kusema hivyo ili kumfurahisha mpenzi wake, ajifanye ameridhika ili mumewe ajione kidume wakati hamna kitu.
Mnaofanya hivyo, mjue mnawakosea waume zenu na naweza kusema mnachangia kwa kiasi kikubwa kuwakosesha urijali, kwani akikufanyia manjonjo kidogo ukamdanganya, ujue atazoea na hiyo tabia itamfanya awe mvivu!

Usimdanganye mumeo, kama kuna sehemu ambayo unahisi hakufurahishi mueleze pia muelekeze jinsi ya kukufanya ufurahie haraka.Jiandae kisaikolojia kwani utakayeumia ni wewe, utajikuta unachukia kukutana na mwenza wako, maana kila akikugusa utaona anakusumbua tu!

Madhara ya kudanganya faragha ni mabaya kwani unaweza kumaliza hamu zote za mwili lakini pia unaweza kujikuta umekuwa msaliti, maana itakulazimu kwenda nje kukata kiu yako.
Madhara mengine ni pale mumeo atapokuja kugundua kuwa unamdanganya. Ni rahisi sana kukuacha kwa sababu ataona ulimfanya zuzu wakati yeye alijiamini kwa wakati huo.

Bila shaka mnaodanganya mmenielewa na kabla mumeo hajashtuka, nakuasa kuachana na tabia hii kwani itakugharimu.Kwa leo naishia hapa tuonane wiki ijayo kwa mada nyingine kali zaidi.

Leave A Reply