The House of Favourite Newspapers

Kama Unashindwa Kumdekeza, Atadekezwa na Mwenzio

0

KARIBU Alhamisi ny­ingine mpenzi msomaji wa Ulimwengu wa Mahaba, nikushukuru kwa maoni na ushauri wako iwe kwa SMS au kunipigia simu.

Mpenzi msomaji kama una mpenzi wako na ukashindwa kumbembeleza basi tegemea kubembelezewa na wanaume au wanawake wenzio.

Angalia usije ukaishia ku­lalamika kila siku kuwa kila mpenzi unayekuwa naye unaibiwa, unapokonywa au anakuacha bila kujua sababu ya kuachwa kwako.

Penzi ni kitu kimoja laini sana ambacho wala huwezi kukielezea au kukishika. Na hata utamu wake ni mtamu ila huwezi kumuelezea mtu akauelewa uhalisi wa utamu wa penzi unaoumaanisha.

Hata hivyo penzi hilo limekuwa likiwatesa watu wengi sana wakiwemo wapenzi wachumba na hata wanandoa.

Kwa mtu ambaye hafahamu, mapenzi yanahitaji mambo mengi ili kulifanya penzi lako liweze kuendelea kudumu na kuwa bora, moja ya kitu hicho ni kubembelezana iwe kwa mwanaume au mwanamke na inapotokea huna muda wa kumbem­beleza mpenzi wako basi tegemea kukaribisha usaliti ndani yako.

Hivi jaribu kutafakari kuwa umetoka ka­zini umevurugwa, kichwa kime­jaa msongo wa mawazo ya kazi, maisha na mambo mengine halafu un­afika nyumbani kwa mwenza wako am­baye ulidhani atakuwa sehemu ya kukubembe­leza iwe kwa maneno au vitendo ili kukupunguzia msongo ulionao lakini yeye anaonekana yuko bize na hamsini zake, unadhani nini utakuwa unawaza kwenye akili yako.

Ulitegemea kupata faraja kwa mwanamke au mwanaume uliyempenda lakini anakuwa ni sehemu ya kukuongezea mawazo.

Bila shaka utajisikia vibaya na utamuona ni mwanamke au mwa­naume nuksi.

Kama huwezi kumbem­beleza mwenza wako ikatokea akapata mtu am­baye anamjali, anambem

be­leza basi uwezekano wa kusal­itiwa ni mkubwa.

Kubem­belezana kunam­fanya mwenza wako auhisi uhalali wa kukumiliki, ajione yeye ni mwenye bahati kubwa sana ya kupendwa. Unapombem­beleza hata kama kichwa chake kinakuwa kimevurugwa lakini uwepo wako humfanya abadilike na kuchangamka kama hakuna jambo lolote gumu au lililomkwaza.

Katika kubembelezwa huku wanawake ndiyo hasa wanap­enda na wanajua kuwa wanas­tahili wao zaidi kubembelezwa kuliko wanaume.

Kama wewe ni mwanaume hili unapaswa ulifahamu kuwa mwen­za wako anategemea nafasi kubwa zaidi ya wewe kumbembeleza. Inawezekana hukuwa unalijua hili au ulijisahau basi ni vyema ukaelewa somo hili na kuliweka akilini mwako ikiwezekana hata ukalifanya kwa vitendo ili kuboresha uhusiano wako.

Kama ulikuwa hujui kuna wakati

anambem­

mwen­za wako anatamani hata ashinde nawe ndani, mkicheza, mkitaniana, mkikwaru­zana na michezo mingine ya kimapenzi lakini muda huo haupati kutokana na majukumu au maz­ingira yako ya kazi lakini ni vyema ukatenga hata siku yako ya mapumziko kushinda na kufurahia na mwenza wako kuliko kuji­fanya uko bize.

Kama utaendelea na ubize wako ipo siku utakuja kujutia kwani mwenza wako anaweza kufika sehemu akahisi labda pengine huna mapenzi naye, au upendo wako umeanza kuchuja au umepata mchepuko basi na yeye atatafuta mtu wa kumfariji.

Kwa ushauri tembelea ukurasa wetu wa Face­book: Mimi na Uhusiano, Insta:@mimi_na_uhusiano au jiunga na Mi&u What­sApp kwa namba iliyopo hapo juu.

Leave A Reply