The House of Favourite Newspapers

KAMA UNATATIZO LA NGUVU ZA KIUME, HII INAKUHUSU

 

 

UTAFITI wa hivi karibuni nchini Uingereza umebaini tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na ubora wake wake ni kubwa duniani. Imebainika kuwa kati ya jozi tatu za wanandoa moja imeathiriwa na tatizo hilo.Majibu ya tafiti hizi yasiwe sababu ya kukuogopesha, unaweza kuondokana nalo iwapo utazingatia yafuatayo;

  1. A) TUMIA MVINYO MWEKUNDU

Kunywa mvinyo mwekundu kwani unachangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu.Pia unakuondolea uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa.Hivyo, nashauri wenye tatizo watumie kinywaji hiki ni msaada kwao.

  1. B) SPINACHI

Mboga hii ya majani ina asidi ya foliki hivyo ni muhimu katika kuongeza mbegu za kiume. Spinachi na mboga nyingine za majani zenye rangi ya kijani ni muhimu kwa sababu ya vitamini na kuweka sawa usawa wa ‘folate’ kwenye mwili. Kama folate ipo chini kuna uwezekano mwili wa mwanaume ukatengeneza mbegu zisizo na umbile linalotakiwa kwa uzazi na hivyo kusababisha shida ya uzazi kwa mwanamke kama ujauzito hutoka mara tu baada ya mimba kutungwa.

  1. C) BLUEBERRY

Blueberry ni matunda yanayosaidia kuongeza nguvu za kiume. Wengine huyaita ‘viagra asilia’ kutokana na kazi yanayoifanya mwilini. Yana virutubisho vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko wake kuwa mzuri mwilini. Damu ni kila kitu kwenye suala zima la nguvu za kiume.

  1. D) MTINI

Mtini ni matunda yenye kiwango kikubwa cha asidi ya amino ambayo ni kiungo katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ni kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa asidi hii kunaweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.

  1. E) NDIZI

Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamini B ambayo husaidia kuongeza nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo ambacho kinaongeza nguvu za kiume na ashki ya kufanya mapenzi.

  1. F) MAYAI

Mayai ni mbadala wa uhakika katika kuongeza wingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi wakati wa tendo. Mayai yana vitamini E na protini kwa wingi, vitu ambavyo ni muhimu katika kuongeza mbegu. Pia yanafanya kazi muhimu ya kuzipinda seli za mbegu za kiume kutoshambuliwa kirahisi na vijidudu nyemelezi vinavyoweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Comments are closed.