The House of Favourite Newspapers

Kamala Anavyoweza Kumuinua, Kumdidimiza Biden

0

NI  wazi kwamba sasa  chama cha Democratic hakina muonekano wa Joe Biden. Ni chama kinachoashiria ujana na kujumuisha jamii tofauti-tofauti. Ilikuwa wazi kabisa kwamba mgombea wa chama hicho alihitajika kutafuta mtu kijana na pia ambaye sio Mzungu ili kuwa na tiketi inayoashiria watu watakaokipigia kura chama hicho.

 

Harris, ambaye baba yake ni raia wa Jamaica na mama yake ni raia wa India ametimiza kigezo hicho. Amekuwa mwanamke wa kwanza mweusi na wa kwanza raia wa Asia kutafuta nafasi ya juu kupitia chama kimojawapo kikuu. Na ingawa ana umri wa miaka 55, siyo kwamba ni kijana moja kwa moja ila akilinganishwa na Joe Biden, 77, ni mwenye nguvu na ari inayohitajika.

 

Jumanne mchana kabla ya kuteuliwa na Biden, Harris alituma ujumbe kwenye Twitter kuhusu umuhimu wa kujumuisha watu wa jamii mbalimbali katika uongozi wa chama.

 

“Wanawake weusi na wengineo wasio weusi kwa siku nyingi wamekuwa wa uwakilishi wa chini kati ya wanaochaguliwa na Novemba tuna nafasi ya kubadilisha hilo,” aliandika. Imejitokeza kwamba Harris huenda akawa na mchango wa moja kwa moja katika mabadiliko.

 

Kukabiliana na upinzani
Moja ya majukumu ya tangu jadi ya mgombea mwenza wa rais ni kuendeleza kampeni za kuuza sera kwengineko. Makamu wake hufanya kazi ya kukabiliana na upinzani. Ikiwa hili ni moja ya majukumu atakayokuwa nayo Harris, historia inaonyesha kwamba huenda akawa anatekeleza hayo.

 

Biden anakumbuka Harris ndiye aliyemfuata kwa moyo mkunjufu wakati wa mdahalo wa kwanza wa chama cha Democratic Julai 2019, akikosoa hatua yake ya kupinga unyanyapaa katika shule za umma. Aidha, Harris amejidhihirisha kuwa mkakamavu na muuliza maswali mzuri wakati akiwa kwenye Bunge la Seneti.

 

Uimara
Kitu kimoja ambacho wanasiasa ambao wamewahi kuwania ofisi ya umma wamekuwa wakisema kila mara, ni kwamba ni vigumu kuelewa shinikizo lililopo wakati wa kampeni hadi pale utakapokuwa kwenye kinyang’anyiro. Ingawa ndoto ya Harris ya kuwania urais 2020 haikufanikiwa na akajiondoa mapema kabla ya washindani wengine wengi, anajua hali inavyokuwa kwenye mazingira ya kuwania kiti cha ngazi ya urais.

 

Alipoanzisha kampeni yake mbele ya maelfu ya wafuasi wake Januari 2019, alichukuliwa kama mgombea wa juu. Wakati fulani, Julai, baada ya mdahalo wa kwanza aliokuwa amebobea, aliongeza ushawishi wake katika kura za maoni za awali.

 

Harris amepitia changamoto zake na anajua mtu anaweza kukumbana na yapi. Kama angekuwa mtu dhaifu, tayari angekuwa ameshafahamika kufikia sasa lakini almuradi ameamua kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha juu zaidi, inawezekana siku moja Wamarekani wakaanza kumfikiria kama rais.

 

Seneta huyo wa California huenda pia pengine hakuwa mgombea aliyeonyesha msisimko kama mgombea katika kampeni ya 2019, na bila shaka hakuwa karibu na waliotarajiwa kuchukua ushindi, lakini hadi kufikia sasa mchango wake unafahamika. Na Biden naye hadi kufikia sasa anaongoza kwenye kura ya maoni.

 

Changamoto
Kuliko mwengine yeyote anayewania kiti cha makamu wa rais, Harris ana taaluma ya uwanasheria. Katika maandamano ya hivi karibuni kuhusu ukatili unaotekelezwa na polisi na madai ya ubaguzi wa rangi kwenye taasisi, uwepo wa Harris huenda ukalipa suala hili maendeleo makubwa katika chama cha Democratic.

 

Katika maandamano ya hivi karibuni kuhusu ukatili unaotekelezwa na polisi na madai ya ubaguzi wa rangi kwenye taasisi, uwepo wa Harris huenda ukalipa suala hili maendeleo makubwa katika chama cha Democratic.

 

Msemo wa “Harris ni polisi” unaomkejeli ulijitokeza mbele ya seneta huyo wa California zaidi ya mara moja.
Harris kuwa kwenye kinyang’anyiro cha urais kumeonekana kama afueni kubwa kwa mgombea mkuu. Hata hivyo, pia kuna changamoto zake.

 

Harris, akiwa seneta na mwanasheria mkuu wa jimbo, alijaribu kushambulia mrengo wa kushoto wakati wa kampeni yake ya uchaguzi. Alionyesha kupendelea uwepo wa elimu ya bure chuo kikuu, mpango wa mazingira wa kijani kibichi na afya bora kwa wote lakini hakuonekana kuwa na msisimko.

 

Alijikuta amenaswa katika suala la ikiwa bima binafsi inastahili kupigwa marufuku ambalo wengi walikuwa wanalipinga. “Tuondoe yote hayo,” alisema hivyo katika moja ya mahojiano yake. “Tusonge mbele.”

 

Wakati huu, kile ambacho kinaweza kuwa msiba wa kujitakia mwenyewe kisiasa ni kuwa na msimamo mkali wa masuala yanayoegemea siasa – kuonekana kama mtu aliye radhi kubadilisha maadili na imani mradi unaendana na kile tu wanachotaka wapiga kura.

 

Jambo ambalo lilimfanikisha Donald Trump, kwasababu ingawa wafuasi wake hawakukubaliani naye, alionekana kuzungumza kwa ukweli anachofikiria na nia yake.

 

Hatua ya Harris kuonekana kuwa wa mwenye msimamo wa wastani, akabadilika na kufuata mrengo wa kushoto na kurejea tena, pengine kwasababu tu ya Biden huenda kukasababisha baadhi ya wapiga kura wakawa na mashaka na maadili yake.

Leave A Reply