The House of Favourite Newspapers

Kamanda Muliro Atoa Onyo Kali… Hatawavumilia Watakaowasumbua Wafanyabiashara -Video

0

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi halitawavumilia watu watakaowasumbua wafanyabiashara walioamua kufungua maduka yao Kariakoo.

Akiongea leo akiwa Kariakoo Muliro amesema “Kulikuwa kuna taarifa kwamba kuna kikundi cha Watu wachache kinajaribu kuwatisha Watu kwamba wasifungue maduka, tukaona kwamba sasa hapo wanavuka mipaka na kuingilia jukumu letu, suala la kutofungua au kufunga ni suala binafsi”

“Kama kuna Watu wanataka kuendelea na biashara na kufungua maduka yao hawapaswi kutishwa hata kidogo, kila Mtu ana uhuru wa kufanya anachotaka kufanya”

“Sisi tumekuja kuona kwamba kama kuna kikundi kinapita na kuwalazimisha Watu wasifanye biashara, hicho ndio kikundi ambacho itabidi tukihoji kwa kina, ndio maana ukipita baadhi ya maeneo kuna maduka yamefunguliwa na tumewahakikishia usalama”

 

Leave A Reply