The House of Favourite Newspapers

Kamanda wa Jeshi la Polisi Arusha Apata Ajali

Muonekano wa gari alilokuwa akilitumia Kamanda wa Jeshi la Polisi Arusha, Charles Mkumbo.

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amepata ajali katika eneo la Mdori mkoani Manyara baada ya gari alilokuwa akilitumia kusafiria kupasuka gurudumu ‘tairi’ ya nyuma na kupoteza uelekeo.


Kaimu Kamanda wa Polisi, Arusha Yusuph Ilembo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo na kusema gari hilo lililokuwa na watu watatu akiwemo msaidizi wakamanda na dereva, lilipata ajali baada ya kupasuka taili ya nyuma na kupoteza mwelekeo. Mkumbo alipata maumivu kichwani lakini hali zao wote zinaendelea vizuri na wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Mount Meru.

Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Muonekano wa tairi la nyuma baada ya kupasuka.

(HABARI NA GLOBAL RIPOTA – ARUSHA, WHATSAPP 0753 715 770)

 

Comments are closed.