The House of Favourite Newspapers

Kampeni ya Binti CCM kutua Ocean Road

Mwenyekiti wa Binti CCM Kampeni, Debora Charles akizungumza na waandishi wa habari juu ya kongamano lao litakalofanyika katika Hospitali ya Ocean Road jiji la Dar es Salaam
Makamu Mwenyekiti wa Binti CCM Kampeni, Anna Mwalongo akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari juu ya kuwataka mabinti kujitokeza kesho Februari 03 mwaka huu  katika Hospitali ya Ocean Road jiji la Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Binti CCM Kampeni, Debora Charles, amesema kuwa kesho wanatarajia kukutana na wasina na wadau mbalimbali  ili kuweza kuwatia moyo mabinti katika kuhakikisha wanapata elimu mbalimbali hasa kuhusu masuala ya kujitambua na kujua uzalendo wao.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Debora alisema kuwa kesho hiyo kunatarajiwa pia kutolewa huduma mbalimbali za matibabu bure katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ikiwa inaenda sambamba katika kuunga mkono kampeni hiyo ya Binti CCM.

 

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bint CCM Kampeni, Anna Mwalongo aliongeza kuwa  hasa lengo la kukutana kesho ni kuwasaidia wasichana wanaotoka mazingira magumu na kuwa katika mazingira rafiki.

 

 

 

Comments are closed.