The House of Favourite Newspapers

Kampuni ya Azania Kumwaga Zawadi Kibao Msimu Huu wa Sikukuu

0

  

KATIKA msimu huu wa sikukuu, kampuni ya Azania, watengenezaji wa Sabuni za King Limau na Marhaba imetangaza ofa kabambe kwa wateja wake kupitia gazeti hili la Ijumaa Wikienda na Gazeti Ndugu la Ijumaa.

 

 

Zawadi zitakazokuwa zinatolewa zitakuwa ni sabuni za ujazo wa aina mbalimbali, fulana na zawadi nyingine kibao ambazo zitawafanya watumiaji wa sabuni hizo zinazoongoza kwa kuondoa madoa, kutakatisha nguo na kuzifanya zing’are, washerehekee sikuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa furaha.

 

“Namna ya kujishindia zawadi kibao zinazotolewa na Azania Groups of Company, watengenezaji wa Sabuni za King Limau na Marhaba ni rahisi sana! Unatakiwa kuwa unasoma magazeti ya Ijumaa Wikienda na Ijumaa yanayotoka siku za Jumatatu na Ijumaa.

 

 

“Ndani ya kila gazeti kutakuwa na maswali machache na rahisi yanayohusu sabuni za King Limau, Marhaba na Kampuni ya Azania. Kutakuwa na namba maalum ya kutuma majibu kisha wote watakaokuwa wakijibu kwa usahihi, wataingia kwenye droo na washindi watakuwa wakiibuka na zawadi kibao kila wiki,” alisema Catherine Kahabi, mratibu wa shindano hilo litakaloanza Ijumaa ya wiki hii, Desemba 27, 2019 kupitia Gazeti la Ijumaa.

 

Mbali na zawadi hizo, watumiaji mbalimbali wa sabuni mpya za King Limau na Marhaba, wameendelea kushangazwa na maajabu makubwa katika usafi yanayoletwa na sabuni hizo.

 

 

“Mimi ni dobi, huwa nafua nguo hapa kwenye ofisi yangu na kunyoosha, wakati mwingine naenda kuwafulia watu majumbani mwao! Huwa nakwenda na sabuni yangu mwenyewe na chaguo langu limekuwa ni King Limau au Marhaba!

 

“Wote ninaowafulia nguo zao, lazima warudi tena kwangu kutokana na jinsi ninavyozifua nguo zao vizuri! Hizi sabuni ni habari nyingine kabisa,” Mwantumu Daffa, mjasiriamali wa Mabibo jijini Dar es Salaam alimwambia mwandishi wa makala haya wakati wa promosheni ya sabuni hizo inayoendelea mitaani.

 

 

Tofauti kabisa na sabuni nyingine za unga, King Limau na Marhaba, hazichubui kabisa mikono na hii inamuwezesha mtumiaji kufua nguo nyingi bila kuwa na hofu ya mikono yake kuharibika.

 

Pia kiasi kidogo cha sabuni, iinatoa povu jingi ambalo lina uwezo wa kutoa hata yale madoa sugu ambayo yameshindikana kwa sabuni nyingine za kawaida! Uzuri zaidi ni kwamba licha ya kuzitakatisha nguo zako na kuzipa mng’aro wake wa asili, King Limau na Marhaba huziacha nguo zako zikiwa zinanukia vizuri kabisa!

 

 

Namna ya kujipatia sabuni hizo, ni rahisi sana! Nenda duka lolote lililo jirani na mahali ulipo, usiseme sabuni ya unga bali sema King Limau au Marhaba Soap na muuzaji atakupatia kwa bei nafuu kabisa! Kisha baada ya hapo, nenda kaijaribu mwenyewe na utaona matokeo yake!

 

Kwa mawasiliano zaidi, wapigie kwa namba 0710 111 112 au watumie barua pepe kwa anuani ya email: sales@azaniagroup. company.

 

Makala: Mwandishi Wetu, Ijumaa Wikienda

 

Leave A Reply