Injini Mpya Ya “Ge Power” Kupunguza Gharama za Uendeshaji

1461161135122Injini ya gesi ya GE aina ya Jenbacher ambayo itauzwa kwa kampuni ya Said Salim Bhakhresa ili kupunguza gharama za uendeshaji.


Dar es Salaam, Tanzania

Kampuni ya GE ambayo imejikita kwenye biashara ya uvumbuzi na usambazaji wa nishati (NYSE: GE) leo imetangaza kuipa mamlaka Kampuni ya Clarke Energy inayojishughulisha na masuala ya Nishati. Kampuni hiyo ambayo huuza injini hizo kwa niaba ya GE itasambaza injini ya gesi aina ya Jenbacher na itaiuza injini hiyo moja yenye ufanisi wa hali ya juu kwa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (Bakhresa) ili kukamilisha kituo cha kufua Nishati ya joto. Kituo hicho kitasambaza umeme huo kwenye Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha Azam kilichopo Dar es Salaam, Tanzania na hivyo kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji za kampuni hiyo kwa mwaka.

“Sisi tuliwachagua GE pamoja na Kampuni ya Clarke Energy hapa Dar es Salaam kutokana na utendaji wao wenye ufanisi mkubwa katika maeneo mengine nchini Tanzania pamoja na urahisi na upatikanaji wa huduma zao kwa wateja hapa nchini” alisema Rajesh Nair, Meneja Ufundi, Said Salim Bakhresa & Co Ltd.

Tanzania ina akiba kubwa ya gesi ndani ya mwambao wa Pwani na kusini, kumekuwa na mabomba mawili ya gesi ambayo yamejengwa nchini ili kusafirisha gesi kutoka kitovu cha uzalishaji kuelekea kwenye maeneo ya matumizi. Bomba la kwanza lilikamilika miaka michache iliyopita na idadi ndogo ya viwanda na wauzaji wa matumizi binafsi waliunganishwa katika bomba hilo. Bomba la pili la gesi ndiyo limemalizika hivi karibuni na kufungulia fursa ya ununuzi wa gesi kwa viwanda vingi zaidi.

“Bakhresa ni moja ya kampuni inayoongoza katika sekta ya viwanda Tanzania na ufungaji wa mtambo huu wa kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia, utasaidia kupunguza gharama za uendeshaji pamoja na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa,” alisema Hugh Richmond, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Clarke Energy. “Huu ukiwa kama mradi wa kwanza wa kampuni yetu nchini Tanzania, utasaidia kupunguza gharama ya kiwanda kujiendesha huku ukifua umeme wa kuaminika utakaotosheleza mahitaji,” alisema Richmond.

Ufungaji wa mtambo huu utaiwezesha Kampuni ya Bakhresa kutumia gesi hii mpya kupata nishati za umeme na joto kwa ufanisi na uhakika. Kampuni ya Clarke Energy huuza kwa niaba ya GE aina ya injini ya gesi Jenbacher J612 yenye uwezo wa kuzalisha megawati 1.82 (MW) za nishati ya umeme. Mtambo huu utazalisha pia nishati ya joto ambayo itaingizwa kwenye jiko la mvuke lenye uwezo wa kuzalisha kilowati 1,040. Clarke Energy itakua mvumbuzi kwa kuzalisha nishati ya umeme na joto ambapo hili litafanikiwa kwa kufunga mitambo ya umeme kwenye gridi ya taifa ili kuweza kubeba mzigo wa kilovolti 33”.

“Injini za mtambo wa gesi aina ya Jenbacher J612 huzalisha hewa chafu kidogo, ila huzalisha umeme kwa ufanisi wa hali ya juu,” alisema Oluwatoyin Abegunde, Mkuu wa Biashara GE Distributed Power kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa nishati katika Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika. Alisema,” Kwa kuchanganya teknolojia yetu ya uhakika na utaalamu wa Kampuni ya Clarke Energy, kwa pamoja tutazalisha umeme wa uhakika pamoja na suluhisho la kupunguza gharama kwa Kampuni ya Bakhresa na hivyo kuwasaidia kuwa mbele ya viwanda vingine nchini Tanzania.”

Kampuni ya Bakhresa, ni moja ya viwanda vinayoongoza nchini Tanzania na Afrika Mashariki ambayo ilizinduliwa mwaka 1970. Leo hii familia ya viwanda vya Bahkresa imezidi kujizolea umaarufu kibiashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki zikiwamo nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi. Pia nchi za Malawi, Msumbiji na Afrika Kusini. Tayari kuna makampuni kadhaa chini ya mwamvuli wake na imewekeza hasa kwenye sekta ya vinywaji, ufungaji vifaa, huduma za baharini, mafuta ya petroli na burudani.

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment