The House of Favourite Newspapers

Habari za wachumba uliokuwa nao za nini kwa mumeo?

0
Man being tired of arguing with his wife in their living room; Shutterstock ID 90152665; PO: The Huffington Post; Job: The Huffington Post; Client: The Huffington Post; Other: The Huffington Post
Man being tired of arguing with his wife in their living room; Shutterstock ID 90152665; PO: The Huffington Post; Job: The Huffington Post; Client: The Huffington Post; Other: The Huffington Post

Asalaam Alaikum wapenzi wasomaji wangu wa safu hii, bila shaka mu wazima na mnaendelea vema na ujenzi wa taifa hili, kwa wale wagonjwa nawapa pole sana Mwenyezi Mungu atawapa subra na wepesi Ishallah.

Baada ya kusema hayo, leo nimekuja tuongelee suala hili la wapenzi wengi kutoa siri ambazo si nzuri kwa wenza wao.
Hivi inakuwaje hadi unafikia hatua unamwambia mchumba/mke wako wapenzi uliokuwa nao tena siyo mara moja. Leo unamwambia ulishawahi kuwa na f’lani kesho f’lani.

Uhusiano kwa wapendanao unaanzia na usiri kati yenu, sidhani kama ni jambo la busara kueleza uhusiano wako uliopita kwa mkeo/mchumba.

Hivi unapomweleza zamani ulikuwa unatoka na f’lani na kwenda mbele zaidi kwa kumsifia huyo zilipendwa wako kwa utundu wake mlipokuwa kwenye eneo la kujidai unatarajia nini?
Sidhani kama mwenza wako atafurahi badala yake utamkwaza na kukuona humpendi unamkumbuka ‘mtu’ wako wa zamani.
Kama kweli mnapendana na mnataka kufika mbali basi si busara kuanza kumtajia wapenzi uliokuwa nao.

Mada hii imekuja baada ya kupata meseji hivi karibuni kutoka kwa msomaji wa mmoja ambaye jambo hili limemtokea siku chache baada ya kufunga ndoa na kujikuta akiumia sana, msomaji huyo aliniandikia hivi;
“Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 25, nimeoa hivi karibuni lakini cha kushangaza mwenzangu kila inapofika usiku tunapolala anaanza kunisimulia wanaume aliokuwa nao.

“Anawasifia mmoja baada ya mwingine kuhusiana na mambo waliyokuwa wakiyafanya enzi za uhusiano wao, kiukweli naumia sana.”
Kwanza nimpe pole msomaji huyu kwa uvumilivu aliokuwa nao kwani ndivyo mapenzi yanavyotakiwa.
Pili nikurudie wewe mwanamke mwenzangu, ndiyo kwanza umeolewa huna hata muda umeshaanza kumuonesha makucha mumeo tabia uliyokuwa nayo, umeshajiuliza unavyofanya hivyo una kusudio gani?
Hembu badilika, mume uliyenaye hapaswi kujua uhusiano uliokuwa nao awali wala wanaume uliowahi kutoka nao.

Hata kama ulishatembea na wanaume ambao pengine mumeo/mchumba uliokuwa naye anawajua, ibaki kuwa siri yako kwani kufanya hivyo kunahatarisha uhusiano wako.

Jiulize ingekuwa ni wewe unatajiwa wachumba aliotembea nao mumeo ungefurahi?
Katika uhusiano jambo unaloona litamuumiza mkeo/mchumba si vema kumwambia. Sawa labda huyo mpenzi uliyekuwa naye aliwahi kukusaidia kitu f’lani ama alikuwa muhimu kwenye kitu fl’ani ibaki kuwa siri yako moyoni kwa sababu upo katika ulimwengu mwingine, upo katika uhusiano mwingine ambao pengine mmewekeana viapo vya kufa na kuzikana.

Kumbuka uhusiano mpya na bora unatokana na kusahau uhusiano uliopita yaani kutunza siri na siri hizo zinatokana na wewe mwenyewe na mpenzi wako.

Kwa leo niishie hapa naimani wale wote wanaoendelea na tabia hizi wataacha baada ya kusoma hapa na kuelewa. Tukutane tena wiki ijayo kwa mada nzuri.

Leave A Reply