The House of Favourite Newspapers

Kampuni ya Knauf Yatoa Misaada ya Elimu ya Sh.milioni 60 Mkuranga

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Knauf Tanzania, Ilse Boshoff (kulia) akifurahia jambo na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mwanambaya iliyopo Mkuranga mkoani Pwani muda mfupi baada ya kutoa msaada wa madawati 150 na choo chenye matundu 10. Kushotoni Rose Mero ambaye ni meneja rasimaliwatu wa kampuni hiyo.

 

 

SHULE za msingi Kisemvule na Mwanambaya zilizopo Mkuranga mkoani Pwani, zimenufaika na msaada wa madawati 300, matundu kumi ya choo na chumba kimoja cha darasa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 60.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Knauf Tanzania Ilse Boshoff (wa sita kushoto) akiwa katika picha ya Pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Mwanambaya iliyopo Mkuranga mkoani Pwani Pamoja na baadhi ya waalimu na wafanyakazi wa kampuni hiyo muda mfupi baada ya kutoa msaada wa madawati 150 na choo chenye matundu 10 kwa shulehiyo.

 

Msaada huo umetolewa na Kampuni ya Knauf  Tanzania inajihusisha kutengeneza na kuuza vifaa vya ujenzi. Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa kampuni hiyo kusaidia elimu baada ya kusaidia shule za Makangaga na Kiranjeranje zilizopo Kilwa mkoani Lindi mapema mwaka huu.

Meneja Masoko wa kampuni ya Knauf Tanzania Lilian Mangaru (katikati) akipeana mkono na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kisemvule iliyopo Mkuranga mkoani Pwani, Aisha Lussasi muda mfupi baada ya kutoa msaada wa madawati 150 na chumba kimoja cha darasa kwa shule hiyo. Kushoto ni Flora Erasto ambaye ni mwanasheria wa kampuni hiyo.

Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhi misaada hiyo, mkurugenzi wa kampuni hiyo Ilse Boshoff alisema kusaidia maendeleo ya elimu ni moja kati ya vipaumbele muhimu vya kampuni hiyo.

 

Kuwajengea watoto mazingira bora ya kujifunzia ni jambo muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yoyote. Kila mwanafunzi ana haki ya kupata elimu bora na Knauf tunayo furaha kubwa kusaidia maendeleo ya elimu hapa Tanzania kwani jambo.

 

Mkurugenzi huyo alisema Knauf itandelea kuunga mkono jitihada za kusaidia elimu huku ikitilia mkazo  suala la kuwaangalia wanafunzi wa kike. Mwakilishi wa Afisa Elimu Kata, Shizya Mwaweza alisema msaada huo umesaidia kuongeza mahudhurio ya wanafunzi kwa zaidi ya asilia 90.

 

“Baada ya kupata msaada wa madawati haya pamoja na vyoo maudhurio yameongezeka kwa asilimia 90-95. Hii ni kwasababu mazingira yao ya kujifunzia yameboreshwa na wanafurahia kuja shuleni,” alisema

 

Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Mkuranga Veronica Kinyemi alisema madawati hayo yatasaidia wafaunzi 900 kukaa wakati wa kusoma na hivyo kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia.

 

Tunaishukuru sana kampuni ya Knauf kwa msaada huu wa madawati, vyoo pamoja na chumba cha darasa. Hakika utakwenda kuleta tofauti. Nawasihi makampuni na wadau wengine kuunga mkono jitihada za kuboresha kama walivyofanya Knauf,” alisema.

Leave A Reply