The House of Favourite Newspapers

Shirika La Mawasiliano TTCL Lawasaidia Watoto Yatima Kushiriki Pasaka

0

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika kusherehekea Siku Kuu ya Pasaka limetoa msaada wa vyakula pamoja na vinywaji katika vituo vya kulelea watoto yatima na waliopo katika mazingira magumu, ikiwa ni sehemu ya kurejesha sehemu kidogo ya mapato kwa jamii.

Vituo vilivyonufaika na msaada huo ni Kituo cha ‘New Life Orphanas Home’ na Kituo cha ‘Daniel Brother Center’maarufu kama Dogodogo Center – Bunju vyote vikiwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza akikabidhi msaada huo jana, Afisa Uhusiano wa TTCL, Bi. Adeline Berchimance kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Shirika hilo, Mhandisi Peter Ulanga, alisema jukumu la kuwasaidia watoto yatima na walio katika mazingira magumu ni la jamii nzima hivyo kutoa hamasa kwa kila mwenye uwezo na nafasi kushiriki katika kuwasaidia watoto hao.

Alisema jamii ha ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa jamii kusapoti, amewashukuru viongozi wa vituo hivyo kwa moyo wa upendo wanaouonesha kwa watoto hivyo kuzitaka taasisi, mashirika na jamii yote kuwaunga mkono kwa kusaidia baadhi ya changamoto kwenye vituo anuai vya yatima na watoto walioko kwenye mazingira magumu.

Hata hivyo katika hatua nyingine ameiomba jamii kubadilika kwa kuzingatia maadili na kuwa na upendo kwa kila mmoja na familia kuwajibika kwenye suala zima la malezi ili kupunguza watoto wanaokimbilia mitaani.

“Chanzo cha watoto wa mitaani au watoto kukimbilia mitaani kinatokana na wanajamii wote, hivyo endapo kila mmoja atawajibika katika malezi ya watoto tutapunguza kiasi kikubwa hili suala la watoto kukimbilia mtaani au kwenye vituo vya kuwalea,” alisema Bi. Berchimance.

Hata hivyo, aliitaka jamii kuliunga mkono Shirika la TTCL hasa katika huduma mpya ya intaneti ya kasi zaidi kutoka TTCL maarufu kama Faiba mlangoni kwako yanayompa fursa mteja kuperuzi bila kukwama huduma ya intaneti yenye kasi zaidi nchini. #RudiNyumbaniKumenoga.

Kwa upande wao Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha ‘New Life Orphanas Home’, Bw. Kondo Kondo na Mkuu wa Kituo cha ‘Daniel Brother Center’ Dogodogo – Bunju, Fr. Dk. Dyering Maliti wamemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga pamoja na wafanyakazi wote kwa kuonesha moyo wa upendo kwa watoto wahitaji katika vituo hivyo na kuiomba jamii kuungana pamoja kusaidia.

Leave A Reply