The House of Favourite Newspapers

Kampuni ya Vodacom Yatoa Tuzo Kwa Global Publishers

0
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho akiwa na tuzo na cheti cha heshima utoka Kampuni ya Vodacom Tanzania.

Kampuni ya Global Publishers Limited imekabidhiwa tuzo na cheti cha heshima cha kutambua mchango wa ushirikiano kutoka Kampuni ya Vodacom Tanzania.

Global wamekabidhiwa tuzo na cheti hicho katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 20 ya utoaji huduma bora za Vodacom nchini Tanzania iliyofanyika leo Jumanne katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Global Publishers Limited wakiwa katika picha ya pamoja.

Katika sherehe hizo, Vodacom pia ilizindua kampeni yake mpya ya ‘Pamoja Tuyajenge Yajayo’ .

Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi ambaye ndiye aliyekabidhi tuzo hiyo kwa Global na wadau wengine kadhaa waliokuwa na mchango mkubwa wa ushirikiano kwa muda wote wa miaka 20 ya uwepo wao Tanzania, alitoa hotuba aliyoipa jina la tulipotoka, tulipo, na tunapokwenda kuhusu huduma za Vodacom.

“Tunasherehekea miaka 20 ya kuwa karibu na wateja wetu na hasa hasa katika kuboresha na kubadilisha maisha ya Watanzania,” alisema Hendi.

KUHUSU ‘PAMOJA TUYAJENGE YAJAYO’

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi wakati akifafanua zaidi kuhusu kampeni mpya ya ‘Pamoja Tuyajenge Yajayo’ alisisitiza kuwa kampuni yao itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao na wengine watakaendelea kujiunga na Vodacom.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi.

“Tunajivunia miaka 20 ya Vodacom kuweka alama na kuboresha maisha ya Watanzania, kwa pamoja tuyajenge yajayo,” alisema Hisham Hendi na kuongeza:

 

Aidha, sherehe hiyo ilinogeshwa kwa maneno ya busara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Ushirika Vodacom, Bi. Rosalynn Mworia na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Vodacom, Bi. Linda Riwa.

Leave A Reply