The House of Favourite Newspapers

Kamusoko Arejea Mazoezini Yanga

Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini.

KIUNGO mkabaji wa Yanga raia wa Zimbabwe Thabani Kamusoko, baada ya kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili, hatimaye leo ameanza rasmi mazoezi ya pamoja na wenzake ambayo yamefanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kamusoko akipiga tizi.

Kamusoko ameonekana kuwa mwenye ari na nguvu zaidi wakati akifanya mazoezi hayo kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zitakazoendelea kupigwa hivi karibuni baada ya kusimama kwa muda.

Akiendelea kupasha.

 

Mazoezi ya viungo yakiendelea uwanjani hapo.

 

 

NA Musa Mateja | GPL

Comments are closed.