The House of Favourite Newspapers

Kane: Nimefuata Makombe Bayern Afunguka Katika Mahojiano Maalum

0
Harry Kane

MSHAMBULIAJI mpya wa Bayern Munich, Harry Kane amesema amejiunga na klabu hiyo kwa sababu anaona kuna ukaribu wa kushinda makombe sambamba na kufika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa’ tofauti na awali.

Nahodha huyo wa Uingereza alikamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 100 na akacheza kwa mara ya kwanza Jumamosi, akitokea benchi katika mechi ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka RB Leipzig kwenye fainali ya Super Cup ya Ujerumani.

Katika mahojiano yake maalum na Sky Sports News, Kane alisema kwa sasa anajiandaa kwa ajili ya kuanza kwa msimu mpya wa Bundesliga ambapo mabingwa hao watetezi wa ligi hiyo watacheza leo ugenini dhidi ya Bremen.

“Watu wengi huzungumza juu ya mataji na kwa nini nilikuja hapa, lakini hatimaye ilikuwa kuboresha, kupata changamoto mpya na kushinda mataji kila mwaka, kulazimika kufika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa.

“Ikiwa unashinda michezo, ikiwa unashinda mataji, ikiwa unashinda mataji ya Ligi ya Mabingwa na mimi ndiye ninacheza mbele, kuna uwezekano mkubwa kwamba mimi ndiye ninayefunga mabao ambayo hukupa nafasi ya kushinda tuzo zingine za kibinafsi.

“Tuna msimu mrefu mbele. Kuna shinikizo kubwa kwa Bayern Munich kushinda ligi na kufika mbali katika Ligi ya Mabingwa, na hilo ndilo ninalofurahia kujipa changamoto.

“Unapokuwa katika klabu kama Bayern Munich lazima ushinde. Hakuna maswali kuhusu hilo,” alisema Kane na kuzungumzia mechi yake ya kwanza ya Bundesliga leo ambapo Bayern watakuwa ugenuini dhidi ya Bremen.

“Nimefurahi kuanza msimu. Mchezo wowote wa kwanza wa msimu wa ligi ni wa kusisimua kwa sababu uko tayari kwenda na una shauku ya kuonyesha kile unachoweza kufanya.

“Itakuwa mchezo mgumu kama vile kila mchezo utakuwa ugenini, lakini nina furaha kujaribu kuwaonyesha Bayern Munich na kuwaonyesha mashabiki kile ambacho nimekuwa nikifanya maisha yangu yote na kushinda mchezo.”

MORISSON KUISHTAKI YANGA FIFA,MNYAMA AAZA KUTOA KICHAPO BALEKE,ONANA BALAA ,YANGA WATA….

Leave A Reply