The House of Favourite Newspapers

KANISA LA KKKT LAADHIMISHA MIAKA 500 YA MATENGENEZO

0

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), linaungana na waumini wengine wa kanisa la Kilutheri duniani kuadhimisha miaka 500 tangu kufanyika kwa matengenezo ya kanisa hilo yaliyofanyika mwaka 1517 na Martin Luther nchini Ujerumani.

 

Maadhimisho hayo yanafanyika leo Jumapili Novemba 5, 2017 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam yakiambatana na ibada maalumu itakayoongozwa na Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk Alex Malasusa.

 

Maandamano ya kuingia uwanjani yanaongozwa na kwaya ya matarumbeta.

 

Pamoja na waumini wengine, katika maandamano hayo wamo wanafunzi wa kipaimara 3,369 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

 

Akizungumzia maadhimisho hayo hivi karibuni, Msaidizi wa Askofu, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chediel Lwiza alisema ibada hiyo itakuwa ni kumbukumbu ya matengenezo ya kanisa ambayo ndiyo yanayoliongoza sasa.

 

Mchungaji Lwiza amesema ibada itashirikisha sharika 83 na mitaa 243 ikiwa ni maalumu ya kumshukuru Mungu kwa umri mrefu wa kanisa hilo

Leave A Reply