The House of Favourite Newspapers

KANYE ‘KUJENGA’ JUMUIA ISIYOTISHIKA NA JANGA LA MOTO

SIKU kadhaa baada ya ripoti kwamba rapa Kanye West na mkewe Kim, walikuwa wameajiri huduma ya zimamoto kujilinda dhidi ya moto mkubwa wa msituni uliotokea California, rapa huyo ameelezea njia ya kuzuia jumuia isiathirike na moto kama huo. Dhana hiyo ameiweka kwenye akaunti yake ya Twitter Ijumaa Novemba 16.

“Kujenga jumuia isiyofikwa na moto,” ndivyo alivyoandika bila kufafanua ni vipi hilo linawezekana.  Hata hivyo, inaonekana kwao wawili hao linawezekana kwa vile waliweza kuita zimamoto kuja kukabiliana na moto huo ambao ulitia hasara kubwa katika jamii ya jimboni California, Marekani.

Comments are closed.