The House of Favourite Newspapers

Kanye West Asogeza Mbele Tarehe Ya Albam Yake, Zijue Sababu

RAPA Kanye West ametoa sababu za kuchelewa kwa kutoka kwa albam yake mpya  ya ‘Yadhi’ ambayo ilikuwa inategemewa kuingia sokoni Novemba 23 mwaka huu.

 

Kupitia account ya Twitter ya Kanye West ameandika, “Nilijiskia vizuri kuwa jukwani jana usiku na kaka yangu Cudi.  Baada ya kufanya shoo tena, niligundua kwamba albam ambayo nilikuwa naifanyia kazi haikuwa tayari.  Nitatangaza tarehe kamili ya kutoka wakati itakapokamilika.  Nashukuru kwa kunielewa.”

Album ya Yadhi ilikuwa itoke Septemba 29 mwaka huu ambapo alitumia mtandao wa Twitter wa mke wake ‘Kim’ kutangaza hilo lakini ikachelewa mpaka Nov 29.    Lakini wiki iliyopita, Kanye West alisafiri kuelekea Afrika kwa ajili ya kuongezea nyimbo kwenye albam hiyo.

Comments are closed.