The House of Favourite Newspapers

Kanye West, Kim Kardashian Wako Ziarani Uganda

RAPA wa Marekani Kanye West (YE) na mkewe nyota wa masuala ya televisheni, Kim Kardashian West, wamewasili nchini Uganda kwa ziara binafsi yenye lengo la kupromoti utalii.

Hivi karibuni, sekta ya utalii katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, ililaumiwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, kwa kutofanya juhudi za kutosha kupromoti vivutio vya asili nchini humo.

Kanye West arrives Uganda

“Mastaa hao wawili walitua nchini jioni jana katika ndege binafsi,” lilisema gazeti la  Watchdog Uganda la nchini humo Jumamosi iliyopita. Rapa huyo na kundi lake wameweka studio ya muziki ya muda mbugani ambako amepanga kurekodi albam mpya,” iliongeza tovuti ya gazeti hilo.

 

Kim Kardashian na West ambaye amebadili jina lake na kuwa YE, wanasemekana wapo mapumzikoni katika hoteli moja ya kifahari iliyoko karibu na Mto Nile kaskazini mwa nchi hiyo.

Kanye West and Kim Kardashian with kids North, Saint and Chicago

Maprodyuza wa Uganda, Swangz Avenue, wamethibitisha kuwa wanashirikiana na West katika albam yake mpya ya “Yandhi”.

Mnamo Septemba, Museveni aliitaka wizara ya utalii nchini humo na idara ya wanyamapori kuimarisha juhudi za kutangaza utalii nchini humo.

Image result for kanye and kim in uganda

“Utangazaji wa mbuga za wanyama umekuwa ni mdogo sana.  Nchi ambazo hazina cha kuonyesha katika utalii zinapata watalii wengi kuliko Uganda.  Wizara ya Utalii lazima ijitahidi kutangaza utalii nchi za nje,” limesema gazeti la  Kampala Post.

Kim Kardashian and Kanye West

Credit: Aljazeera

Comments are closed.