The House of Favourite Newspapers

Kapombe awaonya Simba kuhusu Kessy

0

Said Ally, Dar es Salaam
KIRAKA wa timu ya Azam, Shomari Kapombe, amepeleka ujumbe mzito kwa viongozi wa timu yake ya zamani ya Simba kuwa endapo wataruhusu kuona beki wao wa kulia, Hassan Kessy, anaondoka ndani ya kikosi hicho watakuwa wamefanya uzembe wa hali ya juu kutokana na umuhimu wa beki huyo kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Mganda, Jackson Mayanja.

Kapombe ambaye mpaka sasa anashika rekodi ya kuwa mfungaji bora kwa upande wa mabeki kwenye ligi akiwa na mabao nane, ameyasema hayo wakati huu ambapo Kessy yupo kwenye mgogoro na klabu yake juu ya kusaini mkataba mpya ambapo beki huyo ameshinikiza apewe Sh milioni 60, ili aweze kuendelea kukipiga ndani ya kikosi hicho.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kapombe alisema kuwa viongozi wa Simba wakae chini na kumuongezea mkataba Kessy kutokana na beki huyo kuonyesha mchango mkubwa na kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wameisaidia timu hiyo kufikia mafanikio waliyonayo sasa hivyo kama wakiruhusu kuondoka kwake itawachukua muda mrefu mpaka kuja kumpata anayefanana naye.

“Nasikia juu ya Simba kutaka kuachana na Kessy, kwa upande wangu nasema viongozi hao watafanya kosa moja kubwa endapo watamruhusu beki huyo kuondoka ndani ya kikosi chao kwa kipindi hiki kwani ni miongoni mwa wachezaji muhimu sana kutokana na kiwango chake anachokionyesha kila anapocheza na hata ukifuatilia amekuwa akitoa asisti nyingi za kufunga kwa washambuliaji wake ikiwemo Hamis Kiiza.

“Lakini ukiachana na jambo hilo Kessy ni miongoni mwa mabeki bora wa kulia kwa sasa kwenye ligi ambapo kwa upande wangu naona ukiniondoa mimi yeye ndiye anayenifuata, ambapo kama kweli watamuuza itawachukua muda mrefu sana kuja kupata beki mwingine ambaye ataweza kufanya majukumu kama yake hivyo mimi nawapa onyo wasijaribu kufanya kitu kama hicho tena wampe mkataba mpya,”alisema Kapombe.

Leave A Reply