The House of Favourite Newspapers

Kashfa nzito

IMG-20151127-WA0000Wasomali wakiwa chini ya ulinzi.

Makongoro Oging’ na Issa Mnally
WAMENASWA! Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa wa Machimbo, Kata ya Segerea, Ilala jijini Dar es Salaam wamewanasa watu 105 raia wa Somalia wakidaiwa kuwa safarini kwenda nchini Afrika Kusini, Uwazi linakupa kwa undani.

Tukio hilo la kushangaza lilitokea saa 11 alfajiri ya Alhamisi iliyopita kwenye nyumba ya kigogo mmoja aliyekuwa mfanyabiashara mkubwa Dar (jina lipo) ambaye ni marehemu. Nyumba hiyo iliyopo Tabata Segerea kwa sasa inasimamiwa na mtoto wa marehemu aitwaye Mariam.

IMG-20151127-WA0002

Polisi wakiwa katika eneo la tukio.

Waadishi wa habari hii walifika eneo la tukio muda mfupi baada ya kukamatwa kwa watu hao ambapo zoezi hilo lilikuwa likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kipolisi Buguruni, Ibrahim Nkindwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata Shule, Bakar Goti baada ya kutonywa kuwepo kwa watu hao katika nyumba hiyo iliyopangishwa kwa Zabibu Umwiza raia wa Burundi ambaye ndiye anadaiwa kuwahifadhi watu hao.

ainabu alikimbia baada ya polisi kufika na silaha za moto.
Kwa mujibu wa shuhuda mmoja, kugundulika kwa Wasomali hao kulifuatia kuwasili kwa lori moja kwenye nyumba hiyo usiku wa saa tisa.

IMG-20151127-WA0008

….Wakiwa kwenye basi la polisi.

“Baada ya lori kufika usiku huo, geti likafunguliwa. Halafu kukaanza kusikika vishindo vya tii…tii…tii! Kumbe jamaa (Wasomali) walikuwa wakiruka chini mmojammoja kutoka kwenye lile lori na kuingia ndani.

“Ndipo jirani mmoja aliamua kutoa taarifa polisi ambao walifika na kuwakuta jamaa wamerundikana ndani kwenye vyumba tofauti. Mia moja na tano ni wengi sana,” alisema shuhuda huyo.

Akaendelea: “Tuna shaka hawa watu, wengine ni Al-Shabaab. Hii hali inatia wasiwasi sana. Je, kama wamepita na silaha nzito na wamezificha sehemu? Itakuaje? Hawa Uhamiaji wa mipakani waangaliwe sana.”

IMG_0928

Nyumba walimokutwa wasomali hao.

Mariam anayesimamia nyumba hiyo, anaishi Magomeni, Dar alipofika alishangaa kwa tukio hilo la mpangaji wake kuwahifadhi watu hao, hasa kutokana na idadi yao kuwa kubwa.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Mariam Mchicha naye alikuwa mstari wa mbele katika zoezi hilo la kamatakamata.

Aliitupia lawama Idara ya Uhamiaji na kusema ina matatizo makubwa kutokana na kuwapitisha au kuwepo kwa uzembe wa kuwabaini watu hatari ambao baadaye wanaweza kuleta matatizo makubwa nchini.

IMG_0930

….Moja ya chumba walichokuwa wakilala.

“Nalipongeza Jeshi la Polisi Buguruni kwa kazi nzuri ya kiupelelezi na kuweza kuwagundua watu hawa, ninapenda kuwaasa wananchi kutoa taarifa katika vyombo vya serikali watu wanaowatilia shaka ili wakamatwe,” alisema kiongozi huyo.

Watu hao walichukuliwa katika basi kubwa la polisi huku likisindikizwa na king’ora hadi Kituo cha Polisi Buguruni kwa mahojiano zaidi.

Comments are closed.