The House of Favourite Newspapers

Kassim Majaliwa Awajulia Hali Mzee King Kiki Na Mkuu wa Wilaya ya Mlele

0
Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama (King Kiki) , wakati alipomjulia hali msanii huyo anayesumbuliwa na matatizo ya pingiri za mgongo, nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ali, Novemba 8, 2020.
Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama (King Kiki) , anayesumbuliwa na matatizo ya pingiri za mgongo, nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ali, Novemba 8, 2020.
Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akimpa pole Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rechal Kasanda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari Wilayani Mlele, Mkoani Katavi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi, Novemba 8, 2020. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera.

 

Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa leo Novemba 8, 2020 amemtembelea na kumjulia hali mwanamziki mkongwe nchini Kikumbi Mwanza Mpango maarufu kama King Kikii, Nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ally, Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Majaliwa alimpa pole Kikii anayesumbuliwa na matatizo ya Mgongo na amemtakia pona ya haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake kama kawaida.
Aidha, Mhe. Majaliwa pia alimjulia hali Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rechal Kasanda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari Wilayani Mlele, Mkoani Katavi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi.
Akizungumza na Mhe. Kasanda, Mhe. Majaliwa alimtakia pona ya haraka ili aendelee na majukumu yake ya kuwatumikia WanaKatavi.
Leave A Reply