The House of Favourite Newspapers

KATE KAMBA AWAPOKEA WANACHAMA 200 WALIOJIUNGA CCM

Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Bi Kate Kamba juzi Jumatatu aliwapokea wanachama zaidi ya 200 waliojiunga na chama hicho katika mkutano ulioandaliwa na tawi la chama hicho Kata ya Ubungo National Housing.

 

 

Kate Kamba akiongea na waliohudhuria hafla hiyo.

Hafla ya kuwapokea wanachama hao ilifanyika hotel ya Royal Njombe iliyopo kata hiyo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kata hiyo na wanachama wakongwe wa chama hicho.

 

 

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar, Simon Mwakifwamba akiongea na wananchi walihudhuria mkutano huo.

Baada ya wanachama hao wapya kujiunga na chama hicho Kate Kamba aliwaapisha na kuwalisha kiapo cha uadilifu katika chama hicho na kato wasikisaliti.

 

 

Wananchi wakishangilia maneno mazuri yaliyokuwa yakiongelewa.

 

Mwakifwamba akiwa katika usikivu wa umakini zaidi wakati Kate Kamba akiongea (hayupo pichani).

 

 

Kate Kamba akimkaribisha CCM mmoja wa wananchi waliojiunga na chama hicho kwenye hafla hiyo na kumpa kadi ya uanachama.

 

Baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na chama hicho wakiwa na kadi zao kusubiri kulishwa kiapo.

 

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ubungo National Housing, William Masanja akiongea kwa msisitizo wakati akiwakaribisha wanachama hao wapya waliojiunga na chama hicho kupitia kata yake.

 

Mjumbe wa NEC ya CCM Mkoa wa Dar, Yusuph Majid naye akiwakaribisha wanachama hao wapya na kuwaambia katu wasikubali kurubuniwa na vyama vingine. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM- Tawi la Ubungo National Housing, Japhet Mwasenga maarufu Mwadada.

 

PICHA : RICHARD BUKOS / GPL   

Comments are closed.