The House of Favourite Newspapers

Katibu Mkuu Wizara Ya Habari Atembelea EFM

0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa na wafanyakazi wa Radio ya Efm alipokitembelea chombo hicho cha habari jana jijini Dar es Salaam. Meneja Mkuu wa Radio Efm, Dennis Ssebo  ni wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Efm, DJ Majizo  ni wa pili kutoka kulia.
Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akiongea jambo.
…Akiongea na wasikilizaji wa EFM.
…Akisalimiana na mfanyakazi wa Efm.

MKURUGENZI wa Mawasiliano wa Redio Efm, Denis Ssebo,  amesema kuwa uongozi wa radio yake upo tayari kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na Serikali lengo likiwa ni kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni za utangazaji ili kufanya kazi kwa kiwango chenye ubora .

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa lengo kubwa la Serikali ni kuwepo kwa ushirikiano mzuri na sekta ya habari nchini.

“Lengo la ziara hii ni kuimarisha uhusiano baina ya Serikali na vyombo vya habari pamoja na kufahamu utendaji wenu wa kazi na namna mnavyosimamia maudhui ya vipindi vyenu mnavyoviandaa,” amesema Prof. Gabriel

Aidha aliongeza kuwa ni jambo jema linalofanywa na watanzania wazawa kuwekeza katika sekta ya habari kwa kuwa dunia ya sasa imetawaliwa na utandawazi kupitia taarifa mbalimbali zinazotolewa zenye lengo la kuhabarisha na kujenga taifa letu.

Kwa upande mwingine Prof. Gabriel amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na uzalendo ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Pia amewataka watumishi wa vyombo hivyo vya habari kujenga utamaduni  wa kufanya kazi kwa kujituma ili kupata matokeo chanya katika soko la ushindani na kuifikia jamii kubwa zaidi katika kutoa habari za uhakikia na zenye usahihi.

Sambamba na hilo Prof. Gabriel amevitaka vyombo hivyo vya habari kuzingatia maudhui yanayoendana na jamii ya Kitanzania pale wanapoandaa vipindi mbalimbali ili kujenga jamii yenye utamaduni mzuri ikiwemo kufanya kazi kimkakati.

Angel Mary Kato Atoboa Siri Nzito Kuhusu BSS, Kumbe Waliachwa Kwenye Mataa

Leave A Reply