The House of Favourite Newspapers

Kauli ya CHADEMA Baada ya Lowassa Kurudi CCM

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuondoka kwa mwanachama wake, Edward Lowassa na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) hakutakuwa na madhara yoyote.

 

Hayo yamesemwa jana Ijumaa Machi 1, 2019 na Katibu Mkuu wa chama hicho kikuu cha upinzani Tanzania, Dk Vicent Mashinji muda mfupi baada ya Lowassa ambaye ni waziri mkuu wa zamani kutangaza uamuzi huo.

 

“Tunamtakia maisha mema huko aendapo yeye ni mtu mzima anajua anachokifanya,” amesema Dk Mashinji.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Iringa Peter Msigwa amesema:Kama kuna jambo la maana kubwa Lowasa amefanyia CHADEMA, ni kuondoka CHADEMA kurudi CCM.

LOWASSA BAADA YA KUREJEA CCM

Comments are closed.