The House of Favourite Newspapers

Kazi Imeanza! Manji Athibitisha Kurejea Rasmi Yanga

Baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuitaka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi ikiwemo ya Manji aliyeandika barua ya kujiuzulu Mei 2017 baraza la wadhamini limetoa tamko.

 

Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Yanga ambaye ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuphu Manji amerejea rasmi.

 

“Kwenye mkutano mkuu ule wa wanachama, ilipigwa kura nani wanamtaka Manji arudi, wajumbe wote 4500 walisema tunamtaka Manji arudi na sisi katika baraza la wadhamini tukasema Manji aandikiwe barua “, amesema.

 

“Tukamuandikia barua na mimi mwenyekiti wa baraza ndiye niliyetia saini, amejibu Manji kwa kifupi anasema, Nimepokea maamuzi ya wanachama wa Yanga, lakini bahati mbaya kipindi nimepokea nipo kwenye matibabu, tarehe 15 Disemba madaktari wanasema nitakuwa nimekamilika, nitaanza kuhudhuria ofisini mara kwa mara kuanzia 15, Januari,” ameongeza Mkuchika.

 

Pia, Mkuchika amesema kuwa klabu hiyo sasa ina mwenyekiti wake ambaye ni Yussuph Manji na suala hilo liko kihalali kwakuwa ni maamuzi ya mkutano mkuu.

“Mwenyekiti karudi, Manji amerudi ametuma barua yake sasa kama amerudi yeye ndiye kiongozi wetu amesharudi na Lingalangala yeye ni kaimu Mwenyekiti,” alisema.

Uchaguzi wa Yanga ulipangwa kufanyika tarehe 13 januari mwakani na fomu zilitangazwa kutolewa TFF na Ofisi ya Yanga.

Comments are closed.