The House of Favourite Newspapers

Kazi Imeanza! Sibomana na Bigirimana Watua Yanga

NI rasmi kwamba Yanga imemalizana na Wachezaji wanne kati ya nane wa kigeni aliopanga kuwasajili Kocha Mwinyi Zahera. Zahera ametamka kwa nyodo kwamba hatabembeleza mchezaji yoyote mwenye mkataba au aliyemaliza kwani anaweza kutimua wote akasajili timu mpya tena ya maana.

 

Kocha huyo alitamka wazi kwamba hata straika, Ibrahim Ajibu na Kelvin Yondani wakitaka waondoke habembelezi staa yoyote kwani Yanga ni timu kubwa.

 

Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra imezipata jana ni kwamba mastaa wapya wakigeni waliosaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja ni winga wa Mukura Victory ya Rwanda, Patrick Sibomana, Lamine Moro ambaye ni beki wa kati kutoka Ghana.

 

Wengine ni mshambuliaji wa APR raia wa Rwanda mwenye asili ya Burundi, Issa Bigirimana aliyepewa jina la Walcott akifananishwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal ya England, Theo Walcott. Pia kuna beki wa kushoto anayesifi ka kwa krosi zenye macho, Erick Rutanga ambaye yeye amejiunga na Yanga akitokea Rayon Sports ya Rwanda.

 

“Uongozi huo umefanikiwa kuwasajili Sibomana, Bigirimana (Walcott), Rutanga wote hao raia wa Rwanda na Lamine ambao wote hao wamesaini mkataba wa miaka miwili.

“Pia, leo (jana) uongozi ulitarajiwa kuwasaini wachezaji wengine wanne wa kimataifa kati ya hao yupo beki wa Guinea, Camara (Mohammed) maarufu kwa jina la Pique,” alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza kuwa kipa wa Kenya, Farouk Shikalo alitarajiwa kusaini jana.

 

WAZAWA MUDA WOWOTE

“Muda wowote usajili wa mabeki wa pembeni wa Lipuli ambao ni Gallas (William Lucian) na Paul Ngalema utakamilika. “Pia, Ally Ally ambaye ni beki wa kati KMC ambaye kocha amempendekeza kwenye usajili wake mpya kwa lengo la kuisuka safu yake ya ulinzi ili iwe imara,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye juzi jioni aliahirisha zoezi la kuwataja wachezaji wapya kama alivyokuwa ameahidi, alisisitiza kwamba ndani ya sikumbili yaani jana na leo Alhamisi usajili wake utakuwa umekamilika.

 

“Kati ya hao wachezaji wapo watakaokuja nchini kusaini mkataba na wale tutakaowatumia mikataba huko kwao kwa njia ya barua pepe, pia nimeacha orodha ya wachezaji watatu wazawa niliopendekeza wasajiliwe wawili kutoka Lipuli na mmoja kutoka KMC,”alisema Zahera Spoti Xtra lilishuhudia Mawakala kibao wakiwa na viongozi wa Yanga kwenye hoteli moja maarufu jijini Dar es Salaam na katika makao makuu ya klabu.

 

MWAKALEBELA ANENA

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema; “Ameacha orodha ya wachezaji wazawa aliopendekeza wasajiliwe, hivyo hivi sasa tunachokifanya ni utekelezaji.” Habari za uhakika pia zinasema kwamba dili la Heritier Makambo na Horoya AC ya Guinea linakamilika leo na mkwanja unaingia kwenye akaunti ya Yanga fasta ili wawalipe mastaa wapya.

 

EXCLUSIVE: Zana Coulibaly, NIYONZIMA, Wawa, Wafungukia UBINGWA Wao!

Comments are closed.