The House of Favourite Newspapers

KEANE MAN UTD, ARSENAL HAZIINGII TOP

GWIJI wa soka, Roy Keane, ameponda kuwa hakuna timu yoyote kati ya Manchester United na Arsenal inayostahili kuingia ndani ya nne bora msimu huu. Keane amesema hayo baada ya kutoridhishwa na ufundi ulioonyeshwa na klabu hizo zilipokutana katika mchezo wa Premier juzi Jumatatu uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, Old Traff ord.

 

Ilichukua dakika 28 ndipo shuti la kwanza langoni likapatikana katika mchezo huo, ikiwa ni rekodi ya shuti lililochelewa zaidi msimu huu katika mechi zote za Premier.

 

Kiungo Scott McTominay, aliifungia United bao la kuongoza sekunde chache kabla ya mapumziko, lakini PierreEmerick

Aubameyang alisawazisha kipindi cha pili baada ya VAR kutengua maamuzi mabovu ya mwamuzi wa pembeni aliyedai straika huyo aliotea.

 

“Tumekuwa tukiangalia mechi za Manchester United na Arsenal na hatuamini jinsi mchezo huu ulivyokuwa mbaya,” alisema kiungo huyo wa zamani wa Manchester United.

 

“Kulikuwa na upungufu wa ubora, wachezaji walionekana kuwa chini ya kiwango, kadi za njano nyingi, hakukuwa na nidhamu. Lakini upungufu wa ubora unatisha, hakika.” Nahodha huyo wa zamani wa Manchester United anaamini kuwa timu zote hizi mbili zitateseka sana kuingia ndani ya top 4 na kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

 

Alipoulizwa ipi itaingia ndani ya top 4, Keane alijibu: “Kwa kiwango cha usiku huu (juzi) – hakuna itakayoingia. “United wanatakiwa kuwekeza lakini ukiangalia kiwango cha usiku huu, West Ham na Leicester ndizo zitakazoingia.”

 

 

Lakini beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher, yeye anaamini Arsenal itaingia nne bora kutokana na utajiri ilionao katika safu ya ushambuliaji. “Nasema Arsenal kwa sababu watapata mabao mengi kupitia kwa Lacazette na Aubameyang,” alisema Carragher wakati akiuchambua mchezo huo.

 

 

 

Comments are closed.