The House of Favourite Newspapers

Kelly Rowland Awaandikia Kitabu Akina Mama Kuwafunda Malezi Bora (‘Whoa, Baby!’)

kelly-rowland-baby

Kelly Rowland amefanya jina lake kuwa kama sehemu ya msaada kwa maisha ya mtoto na amekuwa akiwasaidia hata mama wengine kufanya kwa ukamilifu majukumu yao kwa watoto wao.

Kutokana na kuguswa kwake na maisha ya watoto waishio katika mazingira magumu, Rowland sasa ameandaa kitabu ambacho atakichapa hivi karibu kuelezea majukumu ya mama kwa mwane.

Kulingana na chapisho lake la Machi mwaka huu, Whoa, Baby!: A Guide for New Moms Who Feel Overwhelmed and Freaked Out (And Wonder What the #*@& Just Happened) lililoandikwa na Rowland akisaidiwa nza OB-GYN Dr. Tristan Emily Bickman.

“Mimi na Dr. Bickman tulitaka kubainisha majibu nini cha kutarajia baada ya kuzaliwa. Hakuna aliyeniambia uso kwa uso nini cha kutegemea, kwa hisia au kwa fikra.,” alieleza Kelly. “Lengo kuu la Whoa, Baby! ni kumpa mama  ujasiri na elimu kuhusu nini kinaendelea, na kipi amfanyie mwanaye. Tumefanya kila kitu!”

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 35, ameanika mafunzo hayo yakiaksi na maisha halisi ya mtoto wakemwenye umri wa miaka miwili, Titan Jewell.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.