The House of Favourite Newspapers

Shehe Mkuu Wa Mkoa Wa Dar Atembelea Global Publishers

shehe-mkuu-1Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (katikati) akiwa na wafanyakazi wa Global Publishers juzi alipowatembelea ofisini kwao Bamaga, Mwenge, kutoka kushoto ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti pendwa, Oscar Ndauka, Mwanasheria, Emmanuel Elias,  Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli na Mhariri wa Risasi Jumamosi, Erick Evarist.

shehe-mkuu-6

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) na Mhasibu Mkuu wa Global, Lawrence Kabende (kulia) wakiwa na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar.

shehe-mkuu-2

Kutoka kushoto: Mhariri wa Gazeti ya Ijumaa Wikienda, Sifael Paul, Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Amrani Kaima na wafanyakazi wengine wa Global wakiwa katika picha ya pamoja na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

shehe-mkuu-3

Mhariri wa Championi Jumamosi, Elius Kambili (wa kwanza kushoto), Msanifu Kurasa, Charls Mogella (wa pili kutoka kulia) na Walusanga Ndaki (kulia) wakiwa na wakiwa na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar.

shehe-mkuu-7

shehe-mkuu-8

shehe-mkuu-9

shehe-mkuu-10

shehe-mkuu-4

Wafanyakazi wa Global wakiwa na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar.

shehe-mkuu-12

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar akionyeshwa na wahariri uandaaji wa magazeti yetu.

shehe-mkuu-13

Msanifu Kurasa, Bahati Haule (aliyekaa) akimuonyesha shehe gazeti linavyotengenezwa.

shehe-mkuu-14

Wahariri wakiwa katika picha ya pamoja na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar nje ya ofisi za Global.

shehe-mkuu-16

shehe-mkuu-17

…Wakiagana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar.

shehe-mkuu-18

…Akiondoka katika ofisi ya Global Publishers.

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar, Alhad Musa Salum, amesema wilaya ya Kinondoni inaongoza kwa kufanya maovu mengi.

Akizungumza katika mahojiano maalum yaliyofanywa na Global TV  juzi, shehe mkuu alisema yeye na kamati yake ya amani wamekuwa wakijitahidi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali kukemea maovu.

“Uovu ni jambo lisilokubalika na dini yoyote. Mambo ambayo ni maovu kwa uislamu ni maovu pia kwa wakristu, hivyo kila binadamu anapaswa kufuata njia iliyonyooka na kufuata maamrisho ya mwenyezi Mungu,” alisema shehe huyo.

Aliwaasa watu kuacha zinaa huku akimshauri mwanamuziki maarufu, Diamond na mpenzi wake, Zari kufunga ndoa. “Mimi nipo tayari kuwafungisha ndoa bure, hata gari langu nitalitumia bure ilimradi wakubaliane na Zari awe na mtu wa kumsimamia,”alisema. Aliwahimiza watu wote kuishi kwa kumcha Mungu kwani hakuna ajuaye saa ya kufariki dunia hapa duniani.

Comments are closed.