The House of Favourite Newspapers

KEMMY WA KAOLE AMPA UJUMBE MZITO LULU

0
Julieth Samson ‘Kemmy’.

MUIGIZAJI wa muda mrefu aliyewahi kufanya vyema kwenye anga la maigizo kupitia Kundi la Kaole, Julieth Samson ‘Kemmy’ amemuandikia waraka uliobeba ujumbe mzito msanii wa filamu za Kibongo anayetumikia kifungo cha miaka miwili jela, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.

 

Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.

Katika ujumbe huo, Kemmy aliandika;

“Uchungu wa mwana aujuae mzazi hata kama sio kukubeba tumboni.. Lakini baada ya @drchenitz kugundua kipaji chako alikuleta kaole ukiwa na miaka saba hivi.. Naifahamu kwa sehemu safari yako ya sanaa. Mungu anakupenda hayo unayopitia ni hatua ktk safari ya maisha.. Maisha hayana uzoefu na hakuna anayejua kesho ikoje..

 

“Wale walio kutesa na kuhumiza moyo wako kwa tamaa zao ndio waliokupa wakati mugumu, unaopitia.. Lakini Mungu akukumbuke akufutie hatia na damu ambayo ukukusudia kumwaga ,kama mtoto mikononi mwa mtu mzima aliyelewa, amejaa hasira, na ghadhabu na kipigo mimi kama mama najua ulikuwa ktk hali ya kujitetea na kuokioa uhai wako ndio hayo yakatokea.

 

“Lakini usiogope kabisa Mungu ni mwenye huruma, si mwepesi wa hasira Isaya 1..18 dhambi nyekundu kama damu huzifanya nyeupe kama theruji. Mungu akukumbuke, akusamehe upate nafasi ya kuwasamehe wote waliokuumiza na kujisamehe mwenyewe ukitoka kwenye hilo darasa ukawe na mwanzo mpya.. Mungu alijua hiyo hukumu.. Usione kama adhabu bali darasa..

“Nakuombea uhai ili ukitoka uanze maisha mapya yenye ushindi,  hapo hukushindwa bali utakuwa umeshinda zaidi ya kushinda..

“Mungu akawe ngao yako na msaada tele wakati huu Mgumu.

 

NAKUPENDA BINTI YANGU, MUNGU AKULINDE.”

Lulu anatumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii nguli wa filamu Bongo, Steven Charles Meshack Kusekwa Ngamba Kanumba ‘The Great’ usiku wa kuamkia April 7, 2012.

Matukio kama haya na mengine, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply